Habari za Punde

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI UNICEF NCHINI TANZANIA

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa UNICEF Nchini Tanzania Shalini Bahuguna kwa kiwiko alipofika Ofisini kwake.

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na  Mwakilishi Mkaazi wa UNICEF Tanzania Shalini Bahuguna alipofika Wizarani kwake Mnazimmoja kwa mazungumzo pamoja na kumpa ripoti ya utafiti wa kiafya uliofanywa na shirika hilo.

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na  Mwakilishi Mkaazi wa UNICEF Tanzania Shalini Bahuguna alipofika Wizarani kwake Mnazimmoja kwa mazungumzo pamoja na kumpa ripoti ya utafiti wa kiafya uliofanywa na shirika hilo.

Picha na Makame Mshenga.



Na Rahma Khamis Maelezo.

Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF)  kuhakikisha huduma za afya zinaimarishwa hasa katika kulinda na kuhifadhi haki za watoto.

Hayo yameelezwa na Waziri wa afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui Ofisini kwake Mnazimmoja  baada ya  kukabidhiwa taarifa ya utafiti wa kiafya kutoka kwa Muwakilishi Mkaazi wa UNICEF Tanzania Bi Shalini Bahuguna.

Katika taarifa hiyo imeelezwa kwamba watoto wengi Zanzibar wamekuwa wanakosa haki zao za msingi kutokana na kufanyiwa vitendo viovu jambo ambalo linarejesha nyuma jitihada za kuwalinda.

 Katika taarifa ya utafiti huo, UNICEF imebaini kuwa Zanzibar   kunaupungufu watendaji kwa baadhi ya vitengo na ameishauri Wizara kuhakikisha inajaza nafasi za wafanyakazi waliostaafu ili kutoa huduma kwa ufanisi kwa wagonjwa.

Aidha katika taarifa hiyo UNICEF imeshauri kuimarishwa kitengo cha kinga  ili kuwakinga wananchi na maradhi ya mripuko na kuisistiza kuhamasishwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na maradhi ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara,  kuvaa barakoa na kuendeleza utaratibu wa kukaa kwa kupeana nafasi ambao inaonekana kusahaulika.

Bi. Shalini amesema kuwa Zanzibar bado kunatatizo la upungufu wa damu kwa wajawazito hasa katika maeneo ya Micheweni Pemba jambo ambalo linazoretesha afya ya mama na mtoto na ameitaka wizara ya afya kushughulikia suala hilo ili kuiweka jamii katika hali nzuri ya kiafya.

Hata hivyo Muwakilishi huyo amewataka wazanzibari na Tanzania kwa ujumla kuendelea kuchukua jitihada zaidi katika kuimarisha usafi wa mazingira pamoja na kuhakikisha wanakunywa maji safi na salama ili kulinda afya zao.

Waziri wa afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amemuhakikishia Mwakilishi wa UNICEF kuwa Wizara yake itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na shirika hilo katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora za afya mjini na vijijini.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.