Habari za Punde

HOTUBA YA WAZIRI WA WIZARA YA UTALII NA URITHI KWENYE MKUTANO WA UZINDUZI WA MRADI WA KUJENGEA UWEZO WA KUAJIRIWA WAHITIMU KATIKA SEKTA YA UTALII TAREHE 29 MWEZI JUNI MWAKA 2021, ZANZIBAR

Ø Mkurugenzi wa IMED Foundation – Prof Goodluck Urassa

Ø Ndugu waalikwa,

Ø Wanahabari

Ø Mabibi na Mabwana

Nawasalimu Wote kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa kunialika kama mgeni rasmi katika uzinduzi huu wa mraji wa Feed the Future Advancing Youth unaotekelezwa na IMED Foundation na nimefurahi kuwaona wadau wengi wa sekta ya utalii wamefanikiwa kuhudhuria uzinduzi huu

Aidha, nitoe pia pongezi kwa taasisi ambazo zimekubali kujitolea kuwa sehemu ya Uzunduzi wa Mradi. Nawashukuru sana.

Mabibi na Mabwana

Uchumi wa Zanzibar unategemea sekta ya utalii ambayo inakadiriwa kukua kwa asimilia 10 katika kipindi cha miaka 5 ijayo. Chakula na malazi huchangia asimilia 70 ya shughuli za utalii katika visiwa. Vile vile mchango wa ajira za moja kwa moja kutoka kwenge shughuli za utalii inatajirajiwa kuongezeka kwa asimilia 50 katika miaka 5 ijayo. Utalii huchukua asimilia 14.75 ya ajira zote za kulipwa Zanzibar na huajiri asimilia 60.6 ya wageni wote walioajiriwa Zanzibar. Sekta inachangia karibu 80% ya fedha za kigeni kwa Zanzibar na mchango wake kwenye pato la taifa ni asimilia 27%.

Ndugu washiriki wa mafunzo

Kwa upande wa Zanzibar, Sekta binafsi wamekua  mstar wa mbele katika kutoa huduma za kitalii inaendesha malazi ya watalii, shughuli za baharini, maduka ya zawadi, maduka ya urembo. Mnamo mwaka 2017, karibu asimilia 76% ya kazi za moja kwa moja zilitolewa na hotel 473 zilizoko Zanzibar (ZCT, 2017;RGZ, 2017). Kuna hoteli za nyota tano, nne, tatu, mbili na moja, nyumba za wageni daraja la juu, kati na chini. Baadhi ya hoteli kwenye mnyonyoro wa utalii dunia ikiwemon Serena, Kempinski, Hyatt, Protea, Golden Tulip na Best Western zinawakilishwa Zanzibar.Hoteli chache za nyota 4 na 5 mfano Hotel Verde ambayo umilikiwa na mzawa wa ndani ya nchi. Kuna idadi kubwa ya watoa huduma wa utalii Zanzibar ambao ni pamoja na migahawa, watoa huduma baharini, vituo vya spar na maduka ya urembo

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ina sera kadhaa zilizowekwa za kuongoza  maendeleo ya sekta ya Utalii. Hii ni pamoja na Dira ya 2050, Sera ya Uchumi wa Bluu ya Zanzibar (2020), Sera ya Utalii ya Zanzibar 2017), na Sheria ya Utalii ya Zanzibar (2009). Sera ya Zanzibar ya Mabadiliko ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu (2009), Sera ya Utamaduni (2002), Sera ya Biashara Ndogo na ya Kati (2006), Sera ya Uwekezaji ya Zanzibar (2017) na Sera ya Mazingira ya Zanzibar (2013). Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Mkakati wa Utalii wa Zanzibar unaotoa tathmini kamili na inayoangalia mbele ya sekta hiyo na inapendekeza mabadiliko ya jumla kati ya mengine kuwezesha Zanzibar kutoa ‘uzoefu wa wageni wa kiwango cha ulimwengu na kufanya utalii ujumuishwe zaidi kwa kuimarisha elimu na uhusiano wa nyuma.

Kuanzia 2016, Shirika la Kazi Duniali (ILO) linaunga mkono programu ya kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi katika tasnia ya hoteli inayoendeshwa kwa kushirikiana na Chuo cha Utalii (SUZA), Taasisi ya Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI), Chama cha Waajiri wa Zanzibar (ZANEMA) na Baraza la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar. ZATI pia inaenda program (2018-2022) ya kuboresha biashara za wenyeji zinazohudumia sekta ya malazi na kusaidia vijana kuanza biashara. Feed the Future the Future inatekeleza mradi na ZATI ikilenga kuongeza kiwango cha uwezo wa vijana Zanzibar kushiriki katika ujasiriamali. Vile vile, Benki ya Maendeleo ya Africa imeunga mkono Chuo cha Utalii (SUZA) kuanzisha kituo cha kukuza biashara za vijana kwenye sekta ya utalii.

Mabibi na Mabwana

Ripoti ya hivi karibuni ya Benki ya Dunia ilionyesha kiwango cha ukosefu wa ajira Zanzibar kimefikia  asimilia 14%, asimilia 9 ikiwa juu zaidi kuliko bara. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ukosefu wa ajira unaathiri zaidi vijana. Kiwango cha ukosefu wa ajiri kwa vijana wa Zanzibar wenye umri wa miaka 15 – 24 kinakadiriwa kuwa asimilia 27 ikilinganishwa na asimilia 9 kwa Tanzania Bara kwa rika hilo. Vile vile, kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana wa Zanzibar wenye umri wa 25 -34 kwa Zanzibar kimefikia asilimia 17 ikilinganishwa na asilimia 6 kwa Tanzania Bara

Kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana kulingana na umri na eneo la Pemba na Unguja katika eneo la miji kwa vijana wenye umri 15 -24 ni sawa na asimilia 46 ikilinganishwa na vijijini Pemba na Ungujaa ambao ni asimilia 11 na 21 ambao wengi ni wahitimu wa vyuo vikuu na mafunzo ya ufundi. Wakati sekta inatarajiwa kukua kwa kasi lakini mchango wake katika ajira za kulipwa ni bado upo chini.

Baadhi ya wanafunzi wa mafunzo ya ufundi Zanzibar wanapenda kuanzisha biashara yao baada zao baada ya kuhitimu. Katika utafiti wa wanafunzi 70 kutoka Chuo cha Utalii (SUZA) mnamo mwaka 2018, wanafunzi 18 walisema hawatafuti kazi kwa sababu walitaka kujiajiri, Zaidi ya asimilia 20 ya wanafunzi 18 walikuwa tayari wanafanya biashara zisizo rasmi mfano mgahawa, kuuza nguo na kuendesha mashua. Kutoka chuo kiku kwenda ujasiriamali kwa wengi wa wale wanaopenda ni changamoto kwaa sababu ya njia ndogo ya kuishi hususani mapato, ukosefu wa uzoefu, ukosefu wa kutokujiamini, kutiwa moyo na kupata msaada, mitandao mdogo na mtaji mdogo wa kifedha. Vijana kwa kawaida hawaaminiwi na wakopeshaji kama wateja wenzao kubwa.

Kwa njia ya kipekee napenda kutoa shukrani kwa taasisi ya Feed the Future Advancing Youth (AY) ya Marekani ambayo kwa sasa inafadhili mradi huu.  Naamini mkifanya kazi nzuri kwenye mradi huu kama miradi mengine mliotekeleza, mfadhili huyu atasita kuendelea kufanya kazi na IMED Foundation.

Mabibi na Mabwana

Nchi hii tuna Baraka ya kuwa na idadi kubwa ya vijana wenye nguvu. Nasema ni Baraka kwa sababu kuna mataifa ambayo tatizo lao kubwa kabisa ni kukosa nguvukazi kutokana na wastaafu kuwa wengi kuliko vijana.  Lakini Baraka hii inakuja na changamoto kubwa ya kuweka mazingira ya wawekezaji kuzalisha ajira na hawa vijana kujitengenezea ajira.

Sekta ya Utalii Zanzibar inatoa nafasi kubwa zaidi kwa uzalishaji wa ajira rasmi na zisizokuwa rasmi ikilinganishwa na sekta zingine. Wakati vijana wengi waliohitimu na wasio na ajira au kazi za kiuchumi Zanzibar, wawekezaji katika sekta ya utalii wanapata shida kupata wafanyakazi wenye ujuzi na wenye sifa Zanzibar. Ripoti ya hivi karibuni ya ZATI inaonyesha kuwa asimilia 79 ya wafanyakai wanaofanya kazi katika sekta hiyo wana ujuzi mdogo. Sehemu hii inahusishwa na ukosefu wa juhudi zinazoratibiwa katika ukuzaji wa ujuzi na watendaji wa sekta ya umma na binafsi

Tunatambua kwamba mtaji wa kwanza wa kuajiriwa au kuanzisha shughuli ya kibiashara ni kijana mwenyewe kupitia nguvu, maarifa na kuiongeza kwake. Baada ya kuanza kitu, hata kidogo wengine wanapata kuamini kwamba unaweza kujiongeza kutumia fursa kufanya shughuli ya kibiashara. Nimeshukuru kusikia kwamba idadi kubwa ya vijana 100 watakaochaguliwa kwenye mradi huu watepewa maarifa ya ujuzi wa kuajiriwa na kuajiri na pia kutapata fursa ya mafunzo ya vitendo kwenye mnyororo mzima wa thamani wa sekta ya utalii ikiwemo mahoteli, migahawa n.k.

Ndio maana nimefarijika sana kusikia kwamba Feed the Future Advancing Youth inasaidia kupunguza hili tatizo ya hili la ajiar. Kwanza kwa kufanya kazi na IMED Foundation kutoa mafunzo ya ujuzi kuajiriwa na kujiari kwa wahitimu kutoka Pemba na Unguja ambao wameonyesha ubunifu na ufanisi wa hali ya juu katika safari ya kuandaa na kuendesha biashara ya kulingana.

Pia nimefurahi kusikia kwamba lengo la mradi huu pia ni kuwasaidia vijana kurasimisha biashara zao ZRELA.

Mabibi na Mabwana,

Nimefurahi  pika kusikia kwamba tukio hii imehudhuriwa na taasisi mbalimbali kwenye tasnia ya utalii ikiwemo Zanzibar National Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (ZNCCIA), Zanzibar Association of Tourism Investors (ZATI), Zanzibar Tour Operators Association (ZATO), Zanzibar Tour Guides Association (ZATOGA), Zanzibar Associations of Employers (ZAE) and State University of Zanzibar (SUZA) specifically the Institute of Tourism na wengineo. Taasisi hizi zote ni muhimu sana katika kufanikisha kazi kubwa ya kujenga uwezo wa wahitimu kutumia fursa zilizoko kuzalisha ajira, kujijenga kiuchumi, kuongeza vipato na kuchangia katika kazi kubwa ya kuifanya Zanzibar isonge mbele haraka zaidi.

Mabibi na Mabwana,

Naomba niwapongeza tena Feed the Future Advancing Youth kwa kuleta mradi huu muhimu sana Zanzibar na niushukuru uongozi wa IMED Foundation kwa kunialika na wadau wote kwa kunisikiliza, na nawaahidi kwamba serikali ipo pamoja nanyi katika kazi hii.

Pale mnapohitaji ushauri au msaada wowote kutoka wizarani msisite kutufahamisha, na kila iwezekanavyo, tutawasaidia.

Nawatakia kila la kheri nyote.

Mungu awabariki, Mungu aibariki Tanzania. Asanteni!

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.