Habari za Punde

Meneja Mkuu Mpya wa ZECO Azungumza na Wafanyakazi wa Shirika Hilo Leo

.Meneja Mkuu Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Mhandisi;  Mshenga Haidar Mshenga akisikiliza maoni ya wafanyakazi (hawapo pichani) wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Shirika la Umeme uliofanyika katika ofisi za Shirika Saateni Mjini Unguja.

  Meneja Mkuu Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Mhandisi; Mshenga Haidar Mshenga (katikati) akisikiliza maoni ya wafanyakazi (hawapo pichani) wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Zanzibaer uliofanyika katika ofisi za Shirika Saateni Mjini Unguja.

 Baadhi ya wafanyakazi wa ZECO wakifuatilia kwa makini mkutano na Meneja Mkuu wa ZECO, Mhandisi Mshenga Haidar (hayupo pichani) wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Shirika hilo katika ofisi za Shirika zilizopo Saateni Mjini Unguja.

Na. Haji Chapa-ZECO

WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wametakiwa kufanyakazi kwa maslahi ya Shirika na kuacha majungu ili kulipeleka mbele Shirika hilo.

Akizungumza na wafanyakazi wa Shirika hilo katika ofisi za Shirika la Umeme Saateni ikiwa ni mara ya kwanza tokea kuteuliwa kwake, Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Mhandisi; Mshenga Haidar Mshenga amesema kuwa ni lazima wafanyakazi wafanye kazi kwa bidii ili kuliongezea tija Shirika.

Amewataka wafanyakazi hao kuweka mbele maslahi ya ZECO na sivyenginevyo kwani hilo ndio jambo la msingi lililomleta katika taasisi hiyo.

Amefahamisha kuwa baadhi ya wafanyakazi wanatabia ya kubaguana kwa msingi wa maeneo na makundi hivyo amewataka kuacha tabia hiyo kwani ni dalili ya kulirejesha nyuma Shirika kimaendeleo.

Mhandisi. Mshenga amefafanua kuwa licha ya uwepo wa malalamiko mengi kwa wafanyakazi lakini amewata kakufanya kazi kwa juhudi, maarifa, utii, upendo na uvumilivu ili kuliongezea tija Shirika kwani jamii na taifa linategemea wafanyakazi hao katika kuwapatia huduma bora.

Amewatahadharisha wafanyakazi kuacha kuchanganya baina ya maslahi binafsi na ya Shirika na hata mfumbia macho mtendaji atakayeshindwa kudhibiti matamanio yake na kulitia hasara Shirika kwa kuendekeza mgongano wa kimaslahi.

Mapema wafanyakazi wa Shirika hilo wamemuomba Meneja Mkuu huyo kufuatilia maslahi yao kwani maslahi ni jambo pekee linaloweza kumpatia mfanyakazi ari ya utendaji kazi.

Wamesema kuwa muongozo wa mishahara uliotayarishwa kwa ajili ya Shirika hilo umeacha athari kwa baadhi ya wafanyakazi kwani umepelekea baadhi ya wafanyakazi kuathirika mishahara yao.

Aidha,wafanyakazi hao wamemuomba Meneja huyo kuwashirikisha wafanyakazi katika kila jambo linalohusu maslahi ya wafanyakazi kwani miongozo mingi inayotungwa wafanyakazi wa chini ndio wanaoathirika.

Mkutano huo ni wa kwanza kuzungumza na wafanyakazi wa Shirika hilo kwa Meneja Mkuu huyo tangu ateuliwe na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kushika nafasi hiyo ya umeneja mkuu tarehe 4 Mei, 2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.