Habari za Punde

MWANAMUZIKI MKONGWE NCHINI ISMAIL ISSA MICHUZI AFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

                                   

                                               Ismaili Issa Michuzi

 Dar es Salaam, leo

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ismail Issa Michuzi ambaye ni Kaka yake na Mpigapicha na Blogger mahiri nchini Muhidin Issa Michuzi, amefariki dunia.

Taarifa zimesema IsmIli (61), amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, alikokuwa akitibiwa maradhi ya tumbo.


Ismail aliwahi kuwa mmoja wa Waanzilishi na viongozi wa Bendi ya Dar International chini ya Marijani Rajabu na pia alihudumu kama Katibu wa bendi toka mwanzo wake hadi mwisho. 


Baada ya Dar International kudumaa Ismail alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuingizwa katika Bendi ya Mwenge Jazz kama mpuliza trumpet.

Ismail, alitumikia Jeshi hilo la JWTZ hadi alipostaafu takriban miaka sita iliyopita na kuhamia Tukuyu Mbeya ambako alifanya kazi kwa Muda na Radio Chai Fm.


Kwa mujibu wa taarifa tulizopata, mipango ya mazishi inafanyika Tabata Mawenzi, Dar es Salaam na taarifa kamili za maziko zitatolewa baadae

//Blog ya Taifa ya CCM, inatoa pole sana kwa Mpigapicha na Blogger Muhidin Issa Muchuzi na Ndugu wote, Jamaa na marafiki kwa msiba huu.
Ina Lilah Waina Ilyh raj'uun.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.