Habari za Punde

TAMWA Zanzibar Yawajengea Uwezo Kwa Waathirika wa Matukio ya Udhalililshaji na Watoto Wao Ili Wawe na Uwezo Mzuri wa Kutoa Ushahidi Mahkamani.


Na. Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ.                                                                                                   

Katika hali ya kusikitisha Mama mzazi anaekadiriwa kuwa na umri usiopungua miaka 35 ameleza kusikitishwa kwake na baadhi ya watendaji wa Jeshi la Polisi katika kituo cha Mwera  kudharau kesi ya mtoto wake aliebakwa na kuuwawa mnamo mwaka 2019 huko Mwera Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.                                                                                                                        

Aliyasema hayo katika ukumbi wa TAMWA Tunguu Wilaya ya kati Unguja katika mafunzo maalumu ya kujengewa uwezo kwa waathirika wa matukio ya udalilishaji na watoto wao ili wawe na uwezo mzuri wa kutoa ushahidi Mahakamani.                                                                  

Alisema tukio la kubakwa kwa mara ya pili mtoto wake na kisha kuuwawa lilitokea katika mkesha wa mapinduzi ambapo mtoto huyo na wengine walikua nje kutazama fashfashi zilizokua zinapigwa mjini na ndio mtendaji wa tukio hilo alipopata mwanya wa kutenda tukio hilo lililoacha simazi kwa familia yake.                                                                                                    

‘’Tulimtafuta kwa muda mtoto wangu lakini badae  tukamuona akiwa amelala kifudi fudi huku tumboni mwake akiwa na kisu alichochomwa kilichokua na mpini rangi ya manjano na damu nyigi ziliwa zimemwagika kutoka tumboni mwake ‘’alisimulia huku akiwa analia.                        

Alisema wakati matukio yote mawili yanafanyika waliripoti kituo cha polisi Mwera na kesi kuanza kuskiliza kituoni hapo tangu mwaka 2019 lakini kinachomsikitisha hakuwahi kuitwa polisi wala mahakamani hadi leo hii.                                                                                                      

Alisema licha ya kuwa hana uhakika lakini anaamini kuwa alietenda tukio hilo anamjua na ndio mtu ambae mchana wake alikua na kisu kile kile  ambacho kilitumiwa kuchomwa mtoto wake na kutoa uhai wake.                                                                                                                           

 Alieleza kuwa  kijana huyo baada ya kutokea kwa tukio hilo mara nyingi alikua akijificha na kulala juu ya dari badae familia yake ilimsafirisha kwenda Pemba lakini kwa jitihada walizozifanya wao kama wazazi alikamatwa na kurejeshwa Unguja ingawa siku chache alitolewa nje na jeshi la polisi.


Mama huyo anaeleza licha ya chanagamoto hizo hakuwahi kukata tamaa alikwenda kila muda kituo cha polisi  Mwera kuulizia  lakini hakua akiapata majibu mazuri na badae kuelezwa kuwa anapaswa kuliacha jambo hilo.


Akiendelea kufafanua zaidi alisema wakati hayo yanatendeka siku moja alipokea simu kutoka kwa askarini kituo cha Madema aliemuuliza kwa mshangao kuwa eti kesi yake amefuta jambo ambalo alishangazwa nalo na kumueleza kuwa hajawahi kuwa za jambo hilo.

 ‘’Simu hile ya mpelelezi ilinishangaza sana ndipo niliporudi kwa askari wa mwanzo mwera na kuniambia kesi yangu ameifuta kwani alipokea simu yangu kumtaka aifute jambo ambalo mimi sikuwahi kufanya kwa kuwa damu ya mwanangu iliomwagika siwezi kuiacha ipotee na sitaka tamaa hadi kufa kwangu. ‘’aliongezea.


Akiendelea kufafanua zaidi alisema hakuridhishwa na taarifa hizo ndipo alimpofuata askari wa mwanzo kituo cha polis mwera na badae askari huyo alimtaka radhi kwani alifuta kesi hio kimakosa na kueleza kuwa kuna mtu aliejitambulisha ni yeye aklimpigia simu na kumuamuru kufanya hivyo.


Meneja mkuu wa miradi  TAMWA-ZNZ Ally Ahamed  alisema kuna haja kwa jeshi la polisi na watendaji wengine kujivika koti la ubinadamu wakifahamu kuwa matukio hayo yanaweza kuwakuta hata watoto wao wa kuwazaa.

 Alisema anafahamu kuwa wapo maafisa wa jeshi la polisi wanafanyaka kazi vizuri lakini pia miongoni mwao watu wanaozibeza kesi hizo kwa mazingira wanayoyajua wao wenyewe.

 Alitoa wito kwa kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar kufanya utafiti wa kina hususani katika vituo mbali mbali vya polisi kwani kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu kwa baadhi ya watendaji wa jeshi hilo kuzihujumu kesi z audhalilishaji.

Kwa mara kadhaa kamishna wa jeshi la polisi visiwani hapa Mohamed Hassan Haj aliwahi kukemea baadhi ya maafisa wenye kuhujumu kesi za aina hio na nyengine zote na kueleza kuwa jeshi hilo halitakua tayari kuwaumilia maafisa wake wanaojihusisha na tabia hio.

 

Hata hivyo kamishna huyo alitaka jamii iwapo wanaona wanazungushwa kufuatilia kesi zao wasiridhike badala yake wapande ngazi za juu zaidi kupata ufafanuzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.