Habari za Punde

Naibu Waziri Mhe. mmy Aitaka Jamii Kutowafisha Watu Wenye Ulemavu Wakati wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Takwimu Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walipokutana kwenye semina ya kujadili mustakabali wa ujumuishaji wa Watu wenye Ulemavu kwenye Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano Jengo la Takwimu House, Jijini Dodoma.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Mayasa Mwinyi akieleza jambo wakati wa Semina hiyo.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa akieleza akifafanua jambo kuhusu Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika 2022 wakati walipokutana na Viongozi wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) katika Ukumbi wa Mkutano Jengo la Takwimu House, Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (Mb) walipokutana kwenye semina ya kujadili mustakabali wa ujumuishaji wa Watu wenye Ulemavu iliyofanyika hii leo Juni 24, 2021 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akijadiliana jambo na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa.   
Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Wasiiona (TASODEB) Bw. Devid Shaba akipatiwa taarifa ya matukio mbalimbali yanayoendelea na Mtaalamu wa lugha mguso Bw. Joseph Shaba (kulia) wakati semina hiyo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka 2022 Bw. Seif Kuchengo wakati wa Semina hiyo iliyowakutanisha na Viongozi wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Takwimu Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walipokutana kwenye semina ya kujadili mustakabali wa ujumuishaji wa Watu wenye Ulemavu kwenye Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano Jengo la Takwimu House, Jijini Dodoma.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)


Na: Mwandishi Wetu - Dodoma

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu Mhe.Ummy Ndaliananga,ameitaka jamii kuacha kuwaficha watu wenye ulemavu wakati wa Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwakani.

Kauli hiyo ameitolea leo June 24, 2021 wakati akifungua semina ya iliyolenga kujadili mustakabali wa ujumuishaji wa Watu wenye Ulemavu kuelekea Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Naibu Waziri Ummy amesema kuwa kutokuwa na takwimu sahihi za Watu wenye Ulemavu kumepelekea kuwa na changamoto ya utoaji huduma kwa kundi hilo kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi za kutambua walipo, aina ya ulemavu walionao na mahitaji yao, hivyo ili kuwezesha kupata takwimu sahihi za kundi la watu wenye ulemavu zitakazotumika kutekelezea mahitaji yao kwa ufanisi lazima jamii iache tabia ya kuwaficha.

''Kumekuwepo na vitendo kwa baadhi ya wanajamii kuwaficha watu wenye ulemavu wakati wa kipindi cha Sensa ya watu na makazi, kitendo hicho wanaikosesha serikali kupata takwimu sahihi ambazo zingetumika kuwasaidia katika kero mbalimbali zinazaowakabili'' amesema Mhe.Ummy

Aliongeza kuwa agenda moja wapo katika Malengo ya Maendeleo endelevu 2030 ni kuhusu suala la asiachwe mtu nyuma “Leave no One Behind”. Agenda hii inatilia mkazo suala la kuwa kuwapa kipaumbele wenzetu wenye ulemavu katika shughuli mbalimbali.

“Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika 2022 itachangia kwa kiasi kikubwa kuwa na takwimu sahihi za watu wenye ulemavu nchini kama watu wenye ulemavu watashirikishwa kikamilifu bila mtu yoyote nyuma,” alieleza

Alifafanua kuwa, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu umeelekeza pia uwepo wa takwimu sahihi za Watu wenye Ulemavu kunachangia kujipanga vizuri katika kutoa huduma bora kwa kundi hilo.

Pia ameeleza kuwa Serikali imeendela kuwapa kipaumbele Watu wenye Ulemavu katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ustawi wa Watu wenye ulemavu katika katika kuwaleta maendeleo yenye uwiano katika jamii.

“Kwenye Ilani ya Chama Tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye ibara ya 94 na 95 imeelezea namna serikali inavyowatambua watu wenye ulemavu na imeendelea kusisitiza na kutilia mkazo usawa na haki zao,” alieleza

Sambamba na hayo alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika bajeti yam waka wa fedha 2021/2022 imetenga fedha ya kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la sensa ya wat una makazi nae neo moja wapo litakalosimamiwa ni uwepo wa takwimu za watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa serikali Dk. Albina Chuwa amesema kuwa katika Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwakani, wamejipanga kuhakikisha kila kundi linajumuishwa ili kuwa na takwimu sahihi kwa ajili ya kulisaidia Taifa kutekeleza majukumu yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.