Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amewaapisha Leo Ikulu Viongozi Aliowateua Hivi Karibuni.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bw. Abdalla Mzee Abdalla kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bw.Asaa Ahmad Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amemuapisha Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Assa Ahmad Rashid pamoja na Abdalla Mzee Abdalla ambaye amemuapisha kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.

Hafla ya kuapishwa viongozi hao ilifanyika Ikulu Jijini  Zanzibar ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Mwinyi Talib Haji.  

Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa, Makatibu Wakuu, Viongozi wa dini, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, viongozi wengine wa Serikali pamoja na Wanafamilia.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.