Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Juma Malik Akili (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wakuu wa Wizara yake.
Picha na Makame Mshenga.
N
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Juma Malik Akili, amewataka Manaibu Makatibu Wakuu Wakuu, Wakuu wa Maidara na Vitengo vya Wizara yake wafanye kazi kwa ushirikiano na wawe wazi ili kuondoa changamoto mbalimbali ziliopo ndani ya Wizara hiyo.
Akizungumza mara baada ya hafla ya makabidhiano ya ofisi ya aliekuwa Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango Khamis Suleiman Mwalimu (Shibu), katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo Mjini Zanzibar Katibu Mkuu Juma amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa pamoja na kuwa wazi ili kuiletea mafanikio Wizara hiyo.
Nae Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango mpya Aboud Hassan Mwinyi akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi amewaomba mashirikiano maafisa wakuu wa Wizara hiyo kama walivyokuwa wakimpatia mtangulizi wake ili kuwatumikia wananchi wa Zanzibar.
“ Jamani mimi ni mtu nisiependa ubadhirifu wa mali za umma pia ni mumini wa nidhamu, uwajibikaji na nidhamu ya kazi hivyo nawataka tufanye kazi, sina maana kama mlikuwa hamfanyi kazi’’ alisema Aboud.
Aliwataka watafakari pale ambapo hawakufanya viruri wakati wa Khamis Shibu ambapo na yeye atatumia hiyo fursa ya kuongeza ufanisi wa utendaji kazi hasa ukizingatia wao ndio muhimili tegemezi wa Serikali.
No comments:
Post a Comment