Habari za Punde

Mhe Hemed aishukuru Taasisi ya Hayrat Foundation ya Uturuki kwa kusaidia huduma za jamii Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwagaiya misahafu watoto wa Jimbo la Chaani iliotolewa na taasisi ya Hayrat kutoka Nchini Uturuki.
Makamu wa Pili wa Rais, Mhe Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na watoto wa Jimbo Chaani mara baada ya kutekeleza ibada ya Sala ya Ijumaa katika Masjid Rahmani ulipo Chaani Kubwa
 

Na Kassim Abdi, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemd  Suleiman Abdulla, ameishukuru taasisi ya hayrat Foundation kutokana Nchini uturuki kwa jitihada zao za kusaidia huduma mbali mbali za maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

Mhe. Hemd alitoa pongezi hizo katika hafla ya ugawaji wa misahafu kwa ajili ya  wananfunzi wa madrasa kwa jimbo la chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema serikali inathamini michango inayotolewa na taasisi ya hayrat ya uturuki kutokana na misaada yao ambayo imekuwa ikilenga Zaidi kusaidia huduma za kijamii.

Makamu wa Pili wa Rais alihakikishia Taasisi hiyo kuwa serikali ya Mpinduzi zanzibar itaendelea kuinga mkono  taasisi ya Hayrat pamoja na taasisi nyengine akitolea mfano misaada mbali mbali iliotolewa na Taasisi ya Hayrat ikiwemo kusaidia huduma ya usambazaji wa maji safi na salama pamoja kusaidia katika sekta ya elimu.

Aidha, aliwaomba wazazi, walimu na walezi kuzitmia masihafu hizo vizuri kwa kuwasomesha watato katika madrasa mbali mbali ili kufikia lengo lilokusudiwa la kumjua Allah (SW) na kupata rehma zake.

Nae, mratibu wa shughuli za Hayrati Nchini Tanzania Yussuf Kara alishukuru Makamu wa Pili wa Rais kwa ushirikiano wake katika kufanikisha malengo ya Taasisi yao na kuahidi kuwa Taasisi ya Hayrati itaendelea kushirikiana na Zanzibar ili kuinua Elimu kwa Vijana wa Zanzibar.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Jimbo la Chaani Mhe. Nadir Abdulatif alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa amefarajika sana kutokana na misaada mbali mbali inayotolewa na Taaisisi hiyo kutoka Uturuki ambayo siku zote imekuwa chachu kwa vijana na wananchi wa Zanzibar.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alijumuika na waumini na wananchi wa jimbo la Chaani katika ibada ya sala ya Ijumaa iliosaliwa katika Masjid Rahmani.

Akihutubu kabla ya kutekeleza ibada ya sala ya Ijuma Khatib wa Mskiti huo Sheikh Ali Zubeir Muhamed aliwaasa wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha Amani na Utulivu ili kutoa fursa kwa serikali kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Sheikh Ali Zubeir aliwaomba vijana kuachana na vitendo viovu ikiwemo udhalilishaji pamoja na vitendo vya ubakaji vitendo ambavyo vinakatazwa kupitia dini tukufu ya Kislam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.