Habari za Punde

Mkurugenzi TAMWA-ZNZ ataka waandishi wajikite na habari za haki na uwajibikaji

Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar  (SUZA)Dkt.Mzee Mustafa alipokua akitoa mada katika mafunzo hayo kuhusu umuhimu wa uwajibikaji

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea na majadiliano kabla ya kuwasilisha taarifa za makundi


Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ

Waandishi wa habari visiwani Zanzibar wametakiwa kutambua umuhimu wa haki za kila raia pamoja na kujikita katika kuongeza kasi ya ushawishi wa uwajibikaji kwa taasisi mbali mbali za Serikali pamoja na sekta binafsi.


Kauli hio imetolewa na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari Zanzibar Dkt,Mzuri Issa wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa tofauti kisiwani Unguja yaliolenga kuhusu haki ya raia na uwajibikaji huko katika ukumbi wa TAMWA Tunguu Wilaya kati Unguja.


Alisema  kuwa waandishi wa habari wanawajibu mkubwa kwenye jamii na wanapaswa  kuwekeza nguvu zao ikiwa ni pamoja na  kuhakikisha haki za kila raia zinakuepo na kulindwa wakiamini kuwa kufanya hivyo ni kutekeleza majukumu yao ambayo yataisaidia jamii.


Sambamba na hayo aliwataka waandishi wa habari hao kujijengea utaratibu wa kuhoji pale wanapogundua haki za raia zinakiukwa ama kuvunjwa.


Sambamba na hayo Mkurugenzi huyo akiendelea kufafanua zaidi alsiema waandishi wanawajibu wa kuwajenga wanawake kiuwezo wa kuhoji kuhusu haki zao za msingi ikiwemo usismamizi wa utekelezaji wa miradi inayowalenga wao moja kwa moja.


Akizungumzia kuhusu suala la uwajibikaji Mkurugenzi huyo alisema ipo haja kubwa sana  kwa wanaopewa dhamana kuwajibika ipasavyo wakiamini kuwa uwajibikaji ni chachu ya mabadiliko.


Aidha aliwataka  wanahabari visiwani hapa kutupia jicho miradi inayowahusu zaidi wanawake wakiamini kuwa ni sehemu ya jamii inayohitaji kuungwa mkono hivyo kuendelea kukaa kimya hakutawasaidia wanawake wengi ambao ndio sehemu yenye mchango mkubwa kwa jamii.


Akiwasilisha mada Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt,Mzee Mustafa alisema waandishi wa habari wanadhima kubwa ya kuibadili jamii.


Alisema vyombo vya habari vinapaswa kuishawishi jamii kujitambua kuwa ni sehemu ya watu wanaopaswa kushirikishwa katika mipango mbali mbali ya maendeleo.


Alieleza kuwa iwapo jamii itashirikishwa ni wazi kuwa maendeleo ya haraka yatapatikana sambamba na kuigusa jamii moja kwa moja nayale yote wanayoyahitaji kuweza kutambulika kwa urahisi.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walisema mafunzo hayo yanayolenga uwajibikaji na haki za raia yamekuja wakati muafaka kwao na kuahidi kutafanyia kazi.


Mmoja miongoni mwa waandishi hao ni Salim Kombo Khamis kutoka swahiba FM alisema elimu hio ni mara ya kwanza kuipata na kuahidi kuwa watahakikisha wanafikisha elimu hio kwa jamii kupitia maandiko na vipindi tofauti.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.