Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akutana na Makamisaa wa Sensa ya watu na Makaazi nchini, Ikulu leo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein  Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Kamisaa wa Sensa  ya Watu na Makazi Tanzania Mhe.Anne Makinda, baada ya kumaliza mazungumzo  yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo leo 12/8/2021.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza  Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi  Tanzania Balozi Mohamed Hamza na (kulia kwa Rais) Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi  Tanzania Mhe.Anne Makinda walipofika Ikulu Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo yaliofanyika leo 12/8/2021, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akizungumza na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Mhe.Anne Makinda, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa makabrasha  ya Sensa na  Kamisaa wa Sensa  ya Watu na Makazi Tanzania Mhe.Anne Makinda  baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Ujumbe wake, mazungumzo  hayo yaliofanyika katika ukumbi  wa Ikulu Jijini Zanzibar.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Mhe. Anne Makinda  na Mtakimwi Mkuu wa Zanzibar Bi.Mayasa Mahfoudh  na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Jamal Kassim Ali na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi kutoka Zanzibar.Balozi Mohamed Haji Hamza.
(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.