Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akicheza ngoma za asili za Ivory Coast alipowasili katika mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani jijini Abidan leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiwa katika mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani jijini Abidan nchini Ivory Coast leo. Kulia kwake ni Waziri wa Maendeleo ya Utalii wa nchini Chad Faycal Ramat Issa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Sofitel Hotel jijini Abidan nchini Ivory Coast kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii yanayofanyika leo. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Richie Wandwi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiwasalimia machifu wa makabila mbalimbali ya nchini Ivory Coast katika mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani jijini Abidan nchini leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara ya Utalii ya nchini Ivory Coast katika mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani jijini Abidan leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Richie Wandwi.
No comments:
Post a Comment