Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibarv Mhe.Simai Mohammed Said Amekabidhi Gari Kwa Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe  Simai Mohammed Said, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Hadidi Rashid Hadidi, akiwa katika gari akipunga mkono baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya kuimarisha Elimu Mkoa wa Kusini Unguja, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Afisi ya Mkuu wa Mkoa Tunguu.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe  Simai Mohammed Said  amekabidhi gari pamoja na mafuta lita 2000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.




Na Maulid Yussuf WEMA

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe  Simai Mohammed Said  amekabidhi gari pamoja na mafuta lita 2000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema amekabidhi Gari hiyo  kwa lengo la kusaidia maafisa wa Elimu wa Mkoa huo kufuatilia masuala ya Elimu ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa watoto.

Akizungumza baada ya kukabidhi gari hiyo, Mhe Simai amesema ili waweze kuondokana na kuwa na ufaulu mbovu kwa Wanafunzi wa Mkoa huo, ni lazima uwepo umoja na mashirikiano katika majimbo ya Paje, Chwaka na Uzini.

Aidha amewaomba wawakilishi wa majimbo hayo kuchangia kwa nguvu zote katika masuala ya Elimu, ili kuweza kuinua ufaulu kwa Wanafunzi wao na kuwa mfano mzuri katika Elimu.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini  Unguja Mhe, Rashid Hadid Rashid amempogeza Mhe Simai kwa kuona umuhimu wa Elimu katika Mkoa huo na hivyo  kuamua kuwasaidia Gari watendaji wake kutokana na kuwepo changamoto ya usafiri, ili iweze kusaidia katika ufuatiliaji wa masuala ya elimu.
 
Amesema Mikakati yao katika Mkoa huo ni kuona Elimu inakuwa hivyo ameahidi kuitumia gari hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuitunza ili iweze kudumu na kusaidia katika utendaji wao.

Amewaomba viongozi wa Mkoa huo kuiga mfano kama huo, kwani elimu ni muhimu kwa maisha ya kila siku, na hiyo ni miongoni mwa kuwajali watoto wao.

Gari hiyo imegharimu jumla ya shilingi milioni 10.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.