Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amefungua Mjadala wa Uwekezaji wa Big Breakfast. Ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia wadau wa Uwekezaji Zanzibar wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mjadala wa Uwekezaji wa Big Breakfast, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Mjadala wa Uwekezaji wa ‘Big Breakfast’ ni muhimu sana kwa Taifa kwa Kuzingatia athari za kiuchumi na kijamii zilizojitokeza kutokana na kuwepo kwa janga la Corona Duniani.

Dk. Mwinyi amesema hayo wakati alipozungumza na Wadau mbali mbali wa sekta ya Uwekezaji na Biashara katika Ukumbi wa Hoteli Verde, iliopo Mtoni jijini Zanzibar, katika Mjadala maaalum ‘The Big Breakfasta’ uliolenga kujadili changamoto mbali mbali  zinazojitokeza.

Amesema tangu kuibuka kwa ugonjwa wa Covid -19  Disemba 2019, kumekuwepo athari nyingi za kiuchumi na kijamii na hivyo kuathiri sekta za uzalishaji mali na utoaji huduma nchini.

Alisema hali hiyo imesababisha  kuwepo changamoto mbali mbali  katika sekta za viwanda, kilimo, usafiri wa anga na baharini, hatua iliosababisha kuporomoka kwa sekta ya Utalii  na hivyo kuchochea ogezeko la bei za bidhaa muhimu .

Mapema, Waziri wa Nchi (OR) Uchumi na Uwekezaji Mudrick Ramadhan Soraga alisema lengo la majadala huo ‘The Big Breakfast’ ni kuwakutanisha pamoja wadau kutoka sekta mbali mbali za  Uwekezaji na kujiandaa kimkakati ili kuona namna bora ya kukuza na kuendeleza Uwekezaji nchini, wakati huu Taifa likipitia kipindi cha janga la ugonjwa wa Corona, samamba na kutatua changamoto ziliopo.

Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwezekezaji Zanzibar (ZIPA)  Sharrif Ali Sharrif alisema wadau katika Mjadala huo watapata nafasi ya kuangalia fursa za Uwekezaji zilizopo nchini kupitia sekta mbali mbali,  pamoja na kufahamu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kukuza Uwekezaji nchini.

Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.