Habari za Punde

Taasisi ya Emmy yawafunda wasichana wenye ulemavu

Na Takdir Suweid

 Mkurugenzi wa bodi ya watu wenye ulemavu Zanzibar Ussi Khamis debe amewataka wafadhili na watu wenye uwezo kujitokeza kusaidia miradi ya watu wenye wenye ulemavu ili waweze kujiajiri na kuepuka na hali utegemezi.

 
Akifungua mafunzo ya wiki 2 kwa wasichana wenye ulemavu wilaya ya mjini huko ofisi za jumuiya ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) kikwajuni amesema wanawake wenye ulemavu wanamahitaji makubwa hivyo mafunzo hayo yataweza kuwasaidia kupata kujiajiri.

Amesema watu hao wanauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii iwapo watapatiwa mitaji ya kuendesha miradi yao wanayoianzisha.

Aidha amewataka wanajamii kuacha tabia ya kuowaona kuwa watu wenye ulemavu ni mzigo na mikosi katika familia na badala yake washirikiane katika shughuli za kijamii ili wapate fursa zinazojitokeza.

Kwa  upande wake mwenyekiti wa taasisi ya Emmy enrich artt inayojishughulisha na shughuli za upambaji Amina amran jumanne amesema lengo la kutoa mafunzo hayo Ni kuwasaidia wasichana wenye ulemavu kuweza kuondokana na tatizo , unyonge na udhalilishaji miongoni mwao.

Hata hiyvo amesema taasisi hiyo inakusudia kuendesha mafunzo hayo kwa wilaya zote za Unguja na Pemba kwa kuwajengea mbinu za kujipatia kipato Cha kuwaendesha katika maisha yao ya kila siku na kusaidia familia zao.

Mafunzo hayo ya wiki 2 ya upambaji kwa wasichana 15 wenye ulemavu Kama vile wasioona,albino na viungo yameandaliwa na taasisi ya Emmy enrich artt kwa kushirikiana na jumuiya ya wanawake wenye ulemavu zanzibar (JUWAUZA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.