Habari za Punde

Zaidi ya Shilingi Bilioni 2 Zimelipwa Fidia Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta.

NAIBU Waziri Nishati Stephen Byabato akizungumza leo wakati  Semina ya Wakuu wa Mikoa kuhusu fursa zitakazopatikana kutokana na mradi wa ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.

NA OSCAR ASSENGA,TANGA

NAIBU Waziri Nishati Stephen Byabato amesema kwamba mpaka sasa Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya EACOP wamekwisha kulipa fidia ya Bilioni 2.286 ya ardhi kwenye maeneo ya vipaumbele vya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda Hadi Chongoleani Tanga

Byabato alisema hayo jana mjini Tanga wakati akifungua Semina ya Wakuu wa Mikoa kuhusu fursa zitakazopatikana kutokana na mradi wa ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.

Ambapo alisema kwamba wananchi 351 wamekwisha kulipwa katika maeneo 14 ya vipaumbele vya mradi wanayaita hivyo kwa sababu ni kwenye zile kambi ambapo shughuli mbalimbali zitakuwa zinafanyika.

Alisema ile mkuza au njia ya kupitisha bomba fidia yake itakuja baade kidogo lakini zile Bilioni 2 na milioni 286 ni kwa ajili ya maeneo walioyachagua itafanyika shughuli hii na hii mfano Tanga, Tabora,Manyara na maeneo mengine kama hayo.

Naibu Waziri huyo alisema malipo ya fidia kwenye kwenye maeneo ya mkuza yanatarajiwa kulipwa mwishoni mwa mwaka huu 2021 huku akieleza kwamba ujio wa mradi wa Bomba la Mafuta utafungua fursa ya ajira zaidi ya 10,000 kwa kipindi cha miaka mitatu ya ujenzi.

Hata hivyo alisema Rais Samia Suluhu amekuwa akiwaasa kila wakati kuwa wahakikishe wanawapa elimu wananchi juu ya mradi huu wa bomba la mafuta na namna watakavyoweza kunufaika.

“Hivyo ni matumaini yangu kwamba wadau na wengine kutoka Taasisi binafasi na wananchi wenu mtajipanga kuhakikisha mnazitumia vema fursa kwa lengo la kunufaika kupitia mradi huo”Alisema

Bomba hilo litapita kwenye mikoa 8 ya Tanzania Bara,wilaya 24,Vijiji 257 na Kata 134 na litasafiri umbali wa kilomita 1443 kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Chongoleani huku kilomita 1147 zipo Tanzania.

Awali akizungumza wakati wa semina hiyo,Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini Dastan Kitandula aliishukuru serikali na kuahidi kuwa bunge litaendelea kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha mradi huo unakamilika na kunufaisha Taifa.

“Bunge lipo pamoja na serikali na tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha mradi huu mkubwa ambao utanufaisha Taifa letu na kuleta ajira nyingi kwa wananchi wetu,”alisema Kitandula.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali Naghenjwa Kaboyoka alisema kuwa lengo ni kuhakikisha bomba hilo la mafuta linaifikia Tanzania kama serikali ilivyokusudia.

“Viongozi ambao bomba hili litapita kwao wasimamie vizuri bomba la mafuta katika sehemu linapopita kwani sisi tunasema fedha za walipa kodi na sisi tutakuwa tunasimamia fedha ambazo serikali imepewa wajibu kuzisimamia matumizi yake na sisi tutakuwa jicho kwa wapiga kura wetu watanzania kwa kujua fedha zimetumikaje,”alisisitiza Kaboyoka.

Akitoa salamu za Chama cha mapinduzi Mkoa, Mwenyekiti chama cha CCM Mkoa Tanga Henry Shekifu alisema kuwa Rais Samia ametupa heshima kubwa ya kumteua waziri wa nishati kutoka hapa kwetu Mkoani Tanga.

Shekifu alisema kuwa anawatakia heri ya kufanya vizuri kwa kile wanachokitekeleza kwani ilani yao imejikita katika kutimiza mahitaji ya wananchi hivyo kutokana na chama hicho kukomaa kisiasa hakina wasiswasai ila watendaji ndio wanapaswa kusimamia na kufanyia utekelezaji maendeleo ya wananchi yanayotekelezwa na serikali.

“Tanga ni moja kati ya mikoa tajiri ilikuwa ni Mkoa wa pili katika kuipatia serikali mapato ambapo yalishuka baada ya zao la mkonge kupungua uzalishaji ila kupitia bomba hili la mafuta litaifanya Tanga mbali na kufunguka kiuchumi lakini pia litaifanya Tanga kuwa ya kihistoria,”Alisema Shekifu.

Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa Tanga Adam Malima alisema Tanzania ina miradi mikubwa miwili ikiwemo mradi wa SGR, na Mradi wa Stigglers george ambapo mradi wa tatu ni mradi huo wa baomba la mafuta hivyo ni vyema wakawa na uelewa wa pamoja wa sasa na wabadae lakini pia ipo haja ya wakuu wa mikoa kupata taarifa za maendeleo katika kila hatua inayotekelezwa.

“Tanga tuna miradi mitatu mikubwa ambapo mradi wa kwanza ni wa upanuzi wa bandari ya Tanga, ambao unakwenda kuingia ushindani na bandari ya Mombasa, mradi wa pili ni Airport Tanga, na Reli ambayo ni miradi ya kimkakati na itafungua uwezo wa kupeleka mizigo maeneo mbalimbali ambapo Mikoa zaidi ya 8 itanufaika na miradi hiyo,”alisema Malima.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania} TPDC| James Mataragio alisema shirika hilo litahakikisha kwamba hatua zote za mradi zinakamilika na unafanyika kwa ufanisi mkubwa ili uweze kuleta tija kwa Taifa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.