Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limempandisha katika Mahakama Kuu ya Zanzibar, Khator Said Hamad kwa tuhuma za kumuuwa mkewe Zulfat Sheikhan huko Kianga Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Imedaiwa Mahakamani Hapo mbele ya waendesha mashitaka kwamba mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo mnamo siku ya Jumatatu 20-09-2021 majira ya saa 06:35 asubuhi huko Kianga Wilaya ya Magharibi A.
Mwendesha Mashitaka kutoka afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Said Ali akisaidiana na Mohd Haji wameiambia Mahakama Kuu kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo wameomba wapangiwe tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa.
Kwa upande wa utetezi ukiwasilishwa na wakili msomi, Hassan Kijogoo amesema hawana pingamizi na hilo na wameiomba Mahakama mteja wao apelekwe hospitali kwa ajili ya matibabu.
Nae Jaji Abdul Hakim Ameir Issa, ameihairisha kesi hiyo mpaka tarehe 04-11-2021 kwa ajili ya kutajwa.
No comments:
Post a Comment