Habari za Punde

Kilimo cha Umwagiliaji Kubakabiliana na Athari na Madhara Yatokanayo na Mabadiliko ya Tabianchi.

 Mhandisi, Naomi Mcharo akizungunza na waandishi wa habari hawapo katika picha,, kuhusiana na namna sekta ya kilimo cha umwagiliaji ilivyojipanga katika kukabiliana na athari na madhara yatokananyo na mabadiliko ya Tabianchi.
Picha ikionesha mtambo maarufu kwa jina la kijiko ukifanya kazi katika Skimu ya Kilimo cha umwagiliaji Urumwi mkoani kilimanjaro.


Na MwandishiWetu – Moshi

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imejipanga kimkakati kupitia mpango kambambe wa Taifa wa Umwagiliaji wa mwaka 2018,kukabiliana na athari na madhara yatokanayo na mabadiliko ya Tabia nchi katika sekta ya Kilimo.

Hayo yamesemwa leo mjini Moshi katika maonesho yanayoendelea kuelekea maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani na Mhandisi Naomi Mcharo, kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Mhandisi Naomi amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha ukame na wakati mwingine mafuriko yanayosababisha madhara katika mashamba na uharibifu wa miundombinu ya umwagiliaji, 

“ kwa hivyo sisi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tuna Mpango kabambe ambao tumeanisha kuanzia miaka 10 mpaka 20 yakukabiliana na mabadilio ya Tabianchi,kwamaana ya kwamba tumepanga kuwa na Ujenzi wa mabwawa nchi nzima takribani mabwawa 88, ambayo yapo kimkakatik atika maeneo kame.” Alisisitiza.

Aidha,Mhandisi alibainisha kuwa mabwawa hayo yatajengwa katika maeneo ambayo yanapata ukame kwa muda mrefu na mvua zenye kuleta madhara.

Alibainisha kuwa,maeneo ambayo yatajengwa na yamejengwa mabwawa hayo kama vile katika wilaya ya Kwimba yanasaidia kukabiliana na athari na madhara yatokano na mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Awali Mhandisi Naomi alieleza kuwa, Fedha zinazoingia katika  mfuko wa Taifa wa Umwagiliaji zinatoka katika vyanzo mbalimbali vyamapato,ikiwa ni pamoja na ukodishwaji wa mitambo inayomilikiwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, ambapo fedha hizo zinatumika katika kazi ya matunzo, matengenezo na ujenzi wa Miundombinu katika skimu za kilimo cha umwagiliaji nchini. 

Akitolea mfano wa ukarabati wa skimu ya Pawaga, na Dakawa unaoendelea, Ruaha Mbuyuni ambapo ukarabati wa kingo ya mto Lukosi ulioachanjia umekamilika,na Urumwi Ujenzi unaendelea wa mfumo shirikishi kwa wananchi yaani force account.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.