Habari za Punde

Naibu Waziri Mhe.Mary Masanja Akagua Ujenzi wa Jengo la Hoteli ya Nyota Tatu Burgi-Chato.


Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe. Mary Masanja amekagua ujenzi wa Hoteli ya Kitalii ya nyota tatu  katika eneo la Lubambangwe Burigi Wilayani Chato kwa lengo la kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hoteli hiyo inayotarajiwa kutumika kwa ajili ya watalii watakaotembea  maeneo ya vivutio vya Utalii  Wilayani humo.

Amefanya ziara hiyo ya kushtukiza  jana kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa hoteli hiyo.

Mhe. Masanja amemuelekeza  Mwakilishi wa Mradi huo kutoka TANAPA, Jeremiah Machibya kumsimamishia mkataba mkandarasi huyo kama ameshindwa kumaliza kazi kwa muda unaotakiwa.

"Kama mkandarasi kazi imemshinda tengueni mkataba muweke anayeweza kuimaliza kazi hii kwa wakati" Mhe. Masanja amesisitiza.

Mradi huo wenye gharama ya shilingi Bilioni 11 unaosimamiwa na TANAPA ulianza mwezi Aprili 2020 na ulitarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2021 lakini mkandarasi ameongezewa muda hadi mwezi Machi, 2022 na gharama za ujenzi zilizotumika mpaka sasa ni Bilioni 4.1.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.