Habari za Punde

Kuapishwa Kwa Viongozi Walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Hivi Karibuni.Hafla Iliyofanyika leo Ikulu Zanzibar.


MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla (kushoto) Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Mwanasheria Mkuu Dkt.Mwinyi Talib Haji, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, wakati ukipigwa wimbo wa Taifa na wa Afrika Mashariki kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kwa Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar na Mwanasheria Mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Muumin Khamis Kombo kuwa Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar, hafla hiyo ya uapisho imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 30-10-2021, na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
MHE Muumin Khamis Kombo akiapishwa kuwa Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 30-10-2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bi. Salma Ali Hassan kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said 
Bi.Salma Ali Hassan akiapa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka, akiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla hiyo  ya kuapishwa iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 30-10-2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha.Bi.Mwanamkaa Abdulrahaman Mohammed kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka , hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 30-10-2021
Bi.Mwanamkaa Abdulrahaman Mohammed kiapa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, akiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla hiyo  ya kuapishwa iliyofanyika leo 30-10-2021 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
WAHESHIMIWA Majaji wa Mahkama Kuu Zanzibar wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar na Mwanasheria Mkuu na Naibu Mwanasheria, wakiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar




 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.