Habari za Punde

Kuwepo kwa Shughuli za Chuo cha ‘Africa College of Insuarance & Social Protection’ Kutasaidia Zanzibar Kufanikisha Azma Yake ya Kuwa Kitovu cha Biashara -Dk.Hussein Mwinyi.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisitiza jambo wakati wa mazungumzo na  ujumbe wa Uongozi wa Chuo cha Afrika College Of Insuarance & Social Protection unaoongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Afrika College Of Insuarance & Social Protection Dr.Baghayo A.Saqware (wa pili kulia)   walipofika kujitambulisha Ikulu Jijini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu]

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema  kuwepo kwa shughuli za Chuo cha ‘Africa College of Insuarance & Social Protection’   kutasaidia Zanzibar kufanikisha azma yake ya kuwa kitovu cha Biashara pamoja na masuala mbali mbali ya kiuchumi.

Dk. Mwinyi ametoa hadi hiyo alipozungumza na Uongozi wa Chuo cha Africa College of Insuarance & Social Protection, Ikulu Jijini Zanzibar, ambapo pamoja na mambo mengine uongozi huo umefika kwa ajili ya kukitambulisha Chuo hicho.

Amesema serikali itashirikiana na kufanya kazi pamoja na Chuo hicho na hivyo ipo tayari kuanzishwa kituo cha kuwajengea uwezo wataalamu kwa kuelewa kuwa pamoja na Zanzibar kuwa kitovu cha Biashara, inahitaji kuwa kitovu katika masuala mbali mbali yatakayoimarisha uchumi.

Aidha, Rais Dk. Mwinyik ameridhia ombi la  kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Mashirika ya Bima Afrika unaotarajiwa kufanyika Zanzibar kati ya January 26 hadi 28, 2022 katika Hoteli ya Madinat el Bahari, ambapo washiriki zaidi ya 300 kutoka mataifa mbali mbali Duniani watahudhuria.   

Alisema kufanyika kwa mkutano huo kutatoa fursa kwa washiriki kuona vivutio mbali mbali viliopo hapa  nchini na hivyo kuutangaza Utalii wa Zanzibar.

Nae, Mwenyekiti Mtendaji wa Chuo cha Africa College of Insuarance & Social Protection Dr.  Baghayo Abdalla Saqware aliomba Serikali kushirikiana na Chuo hicho , ili kiweze kuanzisha kituo kitakachofundisha wataalamu katika masuala ya fedha.

Alisema hatua hiyo itatoa fursa kwa Mashirika mbali mbali Duniani kuanzisha Ofisi zao hapa nchini.

Akigusia kufanyika kwa mkutano wa Mashirika ya  Bima Afrika, Saqware alisema pamoja na mamabo mengine, washiriki wa mkutano huo watapata fursa ya kujadili shughuli za kibiashara zilivyofanyika katika mwaka uliopoita (2021).

Chuo cha Afrika College of Insuarance & social Protection kiliopo Jijijini Dar es Salaam,  miongoni mwa malengo yake ni pamoja na kuimarisha elimu, kazi na teknolojia pamoja na kuyatafutia ufumbuzi masuala mbali mbali  katika sekta za fedha na masuala ya kijamii.

Kitengo cha habari,

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.