Habari za Punde

Rais Samia azindua Mwongozo wa Majaji na Mahakimu wanawake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa UN Women hapa Nchini Dkt. Hodan Addou, Balozi wa Sweden Nchini Bw. Anders Sjoberg, Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante O. Gabriel.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, wa pili kushoto Mwakilishi mkazi wa UN Women hapa nchini bibi.  Hodan Addou, kulia Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na Balozi wa Sweden Nchini  Bw. Anders Sjoberg mara baada ya kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia, Ikulu Jijini Dar es SalaamRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Balozi wa Sweden Nchini Bw. Anders Sjoberg, Mwakilishi Mkazi wa UN Women hapa Nchini Dkt. Hodan Addo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello baada ya kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na Balozi wa Sweden Nchini  Bw. Anders Sjoberg mara baada ya kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.