Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Amefungua Ijitimai ya Kimataifa Kijiji cha Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini alipowasili katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa 2021, inayofanyika 22-10-2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini alipowasili katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa 2021, inayofanyika 22-10-2021, katika Markaz hiyo na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua maalum iliyosomwa na Amiri Lulu kutoka Gongolamboto Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi na Amiri Mkuu Ali Khamis Mwalim na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman

WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiitikia Dua ikisomwa na Amiri Lulu kutoka Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar, kabla ya ufunguzi wa Ijitimai ya KimataifaWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa iliofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi, kufungua Ijitimai ya Kimatifa, inayofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Waumini wa Dini ya Kiislam katika hafla ya Ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.