Habari za Punde

Taasisi na Mashirika ya Umma Kuunga Mkono Kitengo cha Benki ya Damu Kuokoa Maisha ya Watu - Mhe Hemed Suleiman.

Makamu wa Pili wa Rais akiwa pamoja na wanamazoezi wengine wakitembea kwa miguu katika Tamasha la mazoezi ya vioungo lilioanzia katika viwanja vya Kombawapya na kumalizia Mao Zedong.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto katika mazoezi ya viungo yaliowashirikisha wanamichezo wa Chama cha michezo (ZABESA) katika viwanja vya Mao Zedong.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed akishiriki katika zoezi la uchangiaji damu kupitia tamasha la mazoezi ya viungo lililoandaliwa na chama cha mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) lililofanyika katika viwanja vya Mao Zeddong.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Wanamichezo baada ya kumaliza matembezi ya mazoezi na mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja.

Na. Kassim Abdi OMPR.

Makaumu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amezihamasisha taasisi za serikali na mashirika binafasfi pamoja na vyama vya michezo kuunga mkono  jitihada za kitengo cha benki ya damu katika kuoka maisha ya watu.

Mhe. Hemed alitoa wito huo katika tamasha la mazozi ya Viungo, lililoanzia katika viwanja vya kombawapya kariakoo kupitia michezani hadi katika viwanja vya Mao Zedong Mpirani.

Makamu wa Pili wa Rais alishiriki katika tamasha la mazoezi ya viungo, lililoandaliwa na chama cha michezo ya viungo Zanzibar (ZABESA) pamoja na vilabu vyengine vya mazoezi Zanzibar.

Akizungumza na wanamazoezi hao aliwakumbusha wananchi kujitokeza kufanya mazozi kwa ajili ya kuimarisha Afya zao, ili kujikinga na maradhi mbali mbali hasa yale yasiombukiza, yanayosababishwa utaratibu mbaya wa ulaji wa vyakula.

Tamasha hilo la mazoezi lililoenda sambamba na zoezi la uchangaji damu, Makamu wa Pili wa Rais aliushari uongozi wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, wazee Jinsia na watoto kwa kushirikiana na kitengo cha damu salama  kuhamasisha Zaidi matamasha ya uchangaji wa damu ili kuisadia jamii wakiwemo kina mama na watoto ambao hihitaji damu kwa kiwango kikubwa wakati wa kujifungua.

Nae waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ahmed Nassor Mazrui, mbali na kuwashajihisha wanamichezo hao kuchangia damu lakini pia aliwashauri kujitokeza kwa wingi kupata chanjo, ili kujilinda na maradhi ya Corona ambayo yamekuwa tishio duniani.

Mhe. Mazrui alisema kinga ya kupambana na maradhi hayo kunahitaji watu wajitokeza kupata chanjo kwani kufanya hivyo kutasaidia kufungua milango mbali mbali hasa masuala ya kiuchumi.

Akisoma risala ya wanamazoezi ya viuongo, Haarith Auni Muhammed alimueleza Makamu wa pili kuwa ZABESA itandaa ratiba maalum kwa ajili ya zoezi la kushajihisha  uchangiaji wa Damu ili kuokoa maisha kwa watu wanaopata ajali, wakiwemo na akina mama na watoto.

Katika risala yao wanamazoezi hao waliomba serikali kuwapatia vijana mafunzo ili yawasaidie kushiriki katika dhana ya uchumi wa Buluu.

Katika Tamasha hilo Makamu wa Pili wa Rais alishiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu pamoja na kutoa wito kwa wananchi wengine kujitokeza Zaidi ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa damu katika hospital.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.