Habari za Punde

RC AWATAKA WAKAZI WA NZEGA KUUNDA UMOJA ILI IWE RAHISI KUPATA FURSA KATIKA MRADI WA MRADI WA EACOP.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(katikati) akiongoza mkutano wa  ndani wa viongozi wa Kijiji cha Sojo wilayani Nzega jana wakati ziara yake ya kufuatilia maandalizi ya awali ya kuanza kazi kwa kusafisha eneo la ujenzi wa Karakana na Kambi katika Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(katikati) akizungumza na viongozi mbalimbali jana alipokuwa na ziara ya kufuatilia maandalizi ya awali ya kuanza kazi za kusafisha eneo la ujenzi wa Karakana na Kambi ya Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki .

Picha na Lucas Raphael, 

Na Lucas Raphael,Tabora.                                                                                                              

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani imewataka Wakazi wa Wilaya ya Nzega kuchangamkia fursa zitazotokana na ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki(EACOP) kwa kuunda Umoja ambao utawawezesha kupata kazi za utoaji wa huduma mbalimbali kwa mafundi.

Kauli hiyo imetolewa jana wakati wa ziara  ya kufuatilia maandalizi ya awali ya kuanza kazi za kusafisha eneo la ujenzi wa Karakana na Kambi ya mradi huo.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inasisitiza kila eneo ambapo kunapotekelezwa mradi wowote wa maendeleo lazima uache neema  kwa wakazi wa eneo lilo jirani na Mradi.theophil

Balozi Dkt. Batilda alisema hali hiyo itasaidia kuongeza  mzunguko wa fedha kwa wakazi wa Wilaya ya Nzega watakaotoa huduma mbalimbali na kuwaletea maendeleo.

Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Batilda aliutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kupima eneo lililo jirani na mradi  kwa ajili ya kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuwepo na viwanja vya wawekezaji ambao watatoa huduma kwa mafundi na vibarua katika mradi huo.

Alisema hatua hiyo itasaidia vijiji vya jirani na mradi kuwa katika mpangilio mzuri na kujengeka kisasa na kuondokana na ujenzi holela wa makazi .

Wakati huo huo Balozi Dkt.Batilda aliwataka Wakulima na wazalishaji wa bidhaa mbalmbali katika maeneo karibu na Mradi huo kuunda umoja ambao utawasaidia kuzalisha bidhaa kwa kiwango cha juu na ubora unaohitaji kwa ajili matumizi ya watumishi wa Mradi huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.