Waziri wa Nishati, Mh.
January Makamba akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mh. Abdulaziz Hamad Alasim, leo Oktoba 18, 2021 katika ofisi za Wizara ya Nishati
jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni Kamishna wa Petroli na Gesi Bw. Michael
Mjinja (kulia) na Bi. Sabra Omar (kushoto) aliyeambatana na Balozi.
Waziri wa Nishati, Mh.
January Makamba akizungumza na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Mh. Hussain
Ahmad Al Homaid, leo Oktoba 18, 2021 katika ofisi za Wizara ya Nishati jijini
Dar es Salaam. Pamoja nao ni Mkalimani Bw. Fawaz Ibrahim Argof aliyeambatana na
Balozi.
Baadhi ya viongozi
walioshiriki kwenye mazungumzo baina ya Waziri wa Nishati, January Makamba na
mabalozi wa nchi za Saudi Arabia, Qatar za Falme za Kiarabu (UAE) wakifuatilia
mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Idara ya
Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Hemedi Iddi Mgaza, Kamishna wa Petroli na Gesi Bw. Michael Mjinja, Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Dkt. James Mataragio na Msaidizi wa
Waziri, Wakili Dunford Mpelumbe.
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akimwelezea jambo
Balozi wa Umoja wa Falme za
Kiarabu (UAE) nchini Tanzania, Mh. Khalifa Abdulrahman M.A Almarzooqi baada ya
kukutana kwa mazungumzo, leo Oktoba 18, 2021
katika ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Aliye pamoja nao
(kushoto) ni Afisa Uhusiano wa Ubalozi, Bw. Saddam Ahmed Ali.
Waziri wa Nishati, Mh. January Yusuf Makamba,
leo Oktoba 18, 2021 kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na
mabalozi wa mataifa ya Saudi Arabia, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na
Algeria nchini Tanzania, kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Waziri Makamba, mazungumzo hayo
yanalenga kuimarisha uhusiano wa kisekta baina ya Tanzania na nchi hizo, ili
kuiongezea tija sekta ya nishati kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
“Rais wetu Mh. Samia Suluhu Hassan yuko
mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta ya nishati inaimarika na kulinufaisha
taifa kiuchumi, hususani katika kuvutia wawekezaji na kutumia vyema rasilimali
za mafuta na gesi asilia,” ameeleza Waziri Makamba.
Mabalozi waliofanya mazungumzo na Mh. Makamba
ni pamoja na Balozi Abdulaziz Hamad Alasim (Saudi Arabia), Balozi Hussain Ahmad
Al-Homaid (Qatar), Balozi Khalifa Abdulrahman M.A Almarzooqi (UAE), na Balozi
Ahmed Djellal (Algeria).
Baadhi ya viongozi waliohudhuria mazungumzo
hayo ni pamoja na Kamishna wa Petroli na Gesi Michael Mjinja, Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Edward
Sokoine na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Dkt.
James Mataragio.
No comments:
Post a Comment