Baadhi
ya watumishi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango wachezaji leo Oktoba 23, 2021
wakati wa maandano ya ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Wizara na Idara za
Serikali Tanzania (SHIMIWI) yanayoendelea mjini Morogoro.
Baadhi
ya watumishi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango wachezaji leo Oktoba 23, 2021
wakati wa maandano ya ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Wizara na Idara za
Serikali Tanzania (SHIMIWI) yanayoendelea mjini Morogoro.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameziagiza
Wizara, Idara, Wakala za Serikali, Taasisi pamoja na Sekretarieti za Mikoa kuweka
utaratibu wa kufanya mazoezi kwa watumishi wote walau mara moja kwa wiki ili
kuimarisha afya zao hatua inayosaidia kuleta tija katika utekelezaji wa
majukumu yao ya kila siku.
Makamu
wa Rais Mhe. Dkt. Mpango amesema hayo leo Oktoba 23, 2021 mkoani Morogoro
alipokuwa akifungua rasmi Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea
mkoani humo.
“Ninawaagiza
Watendaji wakuu wote wa Wizara, Idara, Wakala za Serikali, Taasisi za Serikali
na mikoa yote mhakikishe mnapanga mapema na kutenga bajeti ya masuala ya
michezo na muwaruhusu watumishi wafanye mazoezi mapema ili kujiandaa vyema na
mashindano ya SHIMIWI” amesema Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango.
Ili
kuyafanya mashindano haya kuwa bora zaidi, Dkt. Mpango ameiagiza Wizara ya
Sanaa, Utamaduni na Michezo kupitia Michezo na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
kuendelea kusimamia kanuni za uongozi bora kwa kushirikiana na vyama vya
michezo nchini.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan
Abbasi amewahimiza waajiri wawaruhusu watumishi kushiriki mashindano ya SHIMIWI
kwa kuzingatia michezo ni jambo la kimkakati katika taifa ikiwa ni nguvu laini
ya nchi duniani kote.
Katibu
Mkuu Dkt. Abbasi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapenda na kuwajali
watumishi na inajali na kupenda michezo.
Akizungumza
kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt. Abbasi amemshukuru Mhe.
Makamu Rais kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kuja kufungua mashindano hayo kwa
niaba ya Mhe. Rais na amemhakikishia
kuwa Wizara yake ipo mstari wa mbele katika kusimamia mageuzi makubwa ya
michezo nchini ambapo mafaniko yake yameanza kuonekana katika timu za taifa
zinazoliwakilisha nchi yetu katika michezo mbalimbali kimataifa katika kipindi
kifupi cha Serikali ya Awamu ya Sita.
Miongoni
mwa mafanikio hayo ni hadi sasa timu ya Taifa ya wanaume inaongoza kwenye kundi
lao katika hatua za kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani, timu ya Taifa ya Wanawake
Twiga Stars ni bingwa wa mashindanio ya COSAFA 2021, Timu ya taifa ya Kriketi
ni mabingwa kwa nafasi ya tatu Afrika, timu ya Kriketi ya U-20 waliocheza nchni
Rwanda imeshika nafasi ya tatu Afrika.
No comments:
Post a Comment