Habari za Punde

Ufunguzi wa Mkutano wa Taasisi za Usimamizi wa Mfumo Haki Jinai Pemba.

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Massoud Zahor, akifungua mkutano wa nusu mwaka wa taasisi za usimamizi wa mfumo wa haki jinai Pemba, mkutano uliofanyika kiwanja cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
NAIBU na Kaimu Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Muumini Kombo Juma, akitoa taarifa juu ya mkutano wa nusu mwaka wa Taasisi za usimamizi wa mfumo wa Haki Jinai Pemba, kutano uliofanyika katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba
AFISA Mdhamini Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utawala Bora Pemba, Halima Khamis Ali akizungumza na kumkaribisha mgeni Rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa nusu mwaka wa wa taasisi za usimamizi wa mfumo wa haki jinai Pemba.
MWAKILISHI kutoka shirika la UNDP na Mratib wa Mradi wa kujenga uwezo taasisi za kisheria juu ya upatikanaji wa haki (LEAP) Salma Ali Hassan, akitoa taarifa fupi juu ya mradi huo huko katika ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
WATENDAJI kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashataka Zanzibar, wakifuatilia kwa makini mkutano wa nusu mwaka wa Taasisi za usimamizi wa mfumo wa Haki Jinai Pemba, kutano uliofanyika katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba

WASHIRIKI wa Mkutano wa nusu mwaka wa taasisi za usimamizi wa mfumo wa Haki Jinai Pemba, wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa mkutano huo huko katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.

PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.