Habari za Punde

Waandishi wa Habari Pemba Wapata Mafunzo Umuhimu wa Habari na Amani.

MWENYEKITI wa klabu ya waandishi wa habari Pemba (PPC) Said Mohamed Ali, akiwasilisha mada juu ya umuhimu wa habari na amani, wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari Pemba, kupitia mradi unaojulikana SAUTI YANGU, AMANI YANGU, HATMA YANGU,unaotekelezwa na PPC wakishirikiana na Foundation for civil society na Search for common groud, kwa ufadhili wa umoja wa nchi za ulaya.
MWANDISHI wa habari Fatma Hamad Faki, akiwasilisha kazi za kundi namba tatu wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari Pemba, kupitia mradi unaojulikana SAUTI YANGU, AMANI YANGU, HATMA YANGU,unaotekelezwa na PPC wakishirikiana na Foundation for civil society na Search for common groud, kwa ufadhili wa umoja wa nchi za ulaya.
MWANDISHI wa Habari kutoka gazeti la Zanzibarleo ofisi ya Pemba, Mariyam Salim Habibu akionyesha moja ya chupa zinazohifadhiwa moja ya vilevi watumiaji wake huzitupa njiani na watoto kuokota, chupa ambayo inaweza kusababisha mgogoro baina ya jamii na watumiaji wa vinywaji hivyo.

WAANDISHI wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari Pemba, wakiwa katika kazi za vikundi katika mafunzo kupitia mradi unaojulikana SAUTI YANGU, AMANI YANGU, HATMA YANGU,unaotekelezwa na PPC wakishirikiana na Foundation for civil society na Search for common groud, kwa ufadhili wa umoja wa nchi za ulaya.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.