Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Amezindua Wiki ya Vijana Kitaifa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa Nyaraka na Maktaba ya Mwalimu Nyerere katika Taasisi ya Mwalimu Nyerere Sophia Fredy  ( kulia)  wakati alipotembelea mabanda katika uzinduzi wa wiki ya vijana kitaifa Chato, Geita Oktoba 12, 2021.  Wa pili kushoto ni Karani wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Habiba Nassoro
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mafawidhi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ,Usekelege Nahshon wakati alipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika uzinduzi wa wiki ya vijana kitaifa kwenye uwanja wa Mazaina Chato, Geita Oktoba 12, 2021.  Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama na watatu kushoto Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa  wakati alipotembelea mabanda katika uzinduzi wa wiki ya vijana kitaifa kwenye uwanja wa Mazaina, Chato, Geita Oktoba 12, 2021.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.