Habari za Punde

Kuna umuhimu mkubwa kuhifadhi mazingira na kuyatunza

 Na Ali Issa Maelezo 18/11/2021

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwaza wa Rais Zanzibar Dk. Saada Mkuya Salum amesema kuna umuhimu mkubwa katika kuyatunza na kuyahifadhi mazingira Zanzibar  ili kuhakikisha ardhi inarudi katika hali ya ubora pamoja na kupunguza maafa.


Hayo ameyasema leo huko Maruhubi katika Ofisi ya Idara ya Mazingira wakati alipokutana na Kamati ya Baraza la Wakilishi inayo simamia ofisi ya viongozi wa kuu wa kitaifa.


Amesema hali ya mazingira ya Zanzibar kiujumla hairidhishi kutokana ma kuharibikakwake  kunakotokana na Mabadiliko ya Tabia nchi pamoja na uharibifu wa mazingira wa kuchimba mchanga kiholela na ukataji miti ovyo na kuzagaa plastiki chafu.


Amesema hali hiyo iimeifanya baadhi ya maeneo kuwa katika hali hatarishi na  kupelekea kutokea mmong’onyoko ya udongo, kutuwama maji kwa wingi,na kusababisha maji ya bahari kupanda juu kwa kikina kikubwa.


Amesema hali hiyo lazima  irekebishwe kwa kupanda miti kwa wingi,kuchimba mchanga kwa kufuata maelekezo ya kitaalamu ili kuinusuru nchi maafa yasiweze kutokea.


Alieleza kuwa katika kupambana na hilo serikali italazimika kujipanga zaidi ili kuyanusuru mazingira ya Zanzibar ambapo kikao kijacho cha Baraza la wawakilishi Serikali itatoa tamko rasmi kuhusu mazingira Zanzibar.


Nae Makamu Mwenyekiti wakamati ya Baraza la Wawakilishi inayo simamiaa ofisi za viongozi wa kuu wa kitaifa, Mtumwa Peya Yussuf alisema kuwa kutokana na halihiyo  ya kuharibika  mazingira italazimika kupanda miti kwa wingi ili kuirejesha ardhi katika asili yake.


Alisema kuwa mchanga utalazimika kuchimbwa kwa kufuata maelekezo ya  kiutalam,miti isikatwe ovyo,mifuko idhibitiwe kwani bado inaingizwa nchini, na kuweka mikakati kwa waekezaji wanao wekeza katika visiwa  na maeneo mengine ili kuvituza visiwa hivyo.

 

Akitoa tathimini ya mapato na matumizi na  utekelezaji wa mpango wa bajeti Julai hadi Septemba mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mazingira Zanzibar  Sheha Juma Mjaja alisema  Ofisi ya Makamu wa Kwaza wa Rais inakusanya mapato kupitia taasisi moja tu ambayo ni mamlaka ya usimamizi wa mazingira.


Alisema katika kipindi cha Julai hadi Septemba ofisi hiyo ilipanga kukusanya shilingi 42,800,000 kutoka vyazo vyake vya mapato ambavyo ni ada ya Uhifadhi na ukaguzi wa mazingira hivyo hadi kufika septemba jumla ya 42,900,000 zilikusanywa na kuingizwa katika mfuko wa serikali.


Aidha alisema katika kipindi hicho Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ilipanga kutumia shilingi 2,545,513 ambapo shilingi 740,516,249 zilipangwa kwa ajili ya Mishahara na shilingi 1804,996,837 zilipangwa kwa ajili ya matumizi mengineo na jumla ya fedha zilizo patikana  ni shilingi 1,225,222,209 sawa na asilimia 18 ambapo shilingi 818,596,150 zilitumika kwa ajili ya mishahara na 406,636,059 sawa na asilimia 23 kwa ajili ya matumizi mengineo.


Kamati hiyo ilitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Idara ya Mazingira Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu,Tume ya ukimwi,na Ukingo wa Forodhani Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.