Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Mgeni Rasmi Mahafali ya 40 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania viwanja vya Mao Zedung Zanzibar.

Wahitimu wa Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa (Doctor Philosophy) wakiwa katika maandamano wakiingika katika viwanja vya Mahafali ya 40 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania, hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Mao Zedung Jijini Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika Maandamano ya Mahafali ya 40 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania, wakati wa hafla ya hayo yaliofanyika katika uwanja wa Mao Zedung Jijini Zanzibar leo 25-11-2021,Wilaya ya Mjini Unguja na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe.Simai Mohammed Said. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Mahafali ya 40 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung Jijini Zanzibar leo 25-11-2021, na (kushoto kwa Rais) Prof.Deus Ngaruko Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma) na Prof.Elifas Bisanda Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania.
MKUU wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Mhe.Mizengo Peter Pinda akiwatunuku Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Fasafa (Doctor of Philosophy) wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung Jijini Zanzibar, na (kulia kwake) Makamu Mkuu wa Chuo Huria Tanzania Prof. Elifas Bisanda.(Picha na Ikulu)
MKUU wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Mhe Mizengo Peter Pinda akimtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa mhitimu Bakari Ali Mohammed,  wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung Jijini Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja leo 25-11-2021.(Picha na Ikulu)
WAHITIMU WA Shahada ya Udaktari wa Falsafa Chuo Kikuu Huria Tanzania wakishangilia baada ya kutunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Mhe Mizengo Peter Pinda.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika katika uwanja wa Mao Zedung Jijini Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)

WAHITIMU wa Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Miradi (Master of Project Management) wakitunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania.Mhe. Mizengo Peter Pinda.(hayupo pichani) wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung Jijini Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja leo 25-11-2021.(Picha na Ikulu)

 


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.