Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Ahutubia Mkutano Maalum wa Kumpongeza Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia kabla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, kuhutubia katika mkutano maalum wa kumpongeza Rais Mhe Samia ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja leo.2-11-2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alimpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiunga mkono na kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa katika uongozi wa Rais Samia Tanzania imepiga hatua kubwa za maendeleo.

Sambamba na hayo alitoa pongezi kwa Watanzania kwa kuendelea kumuombea dua kwani mambo anayofanya Rais Samia ni makubwa sana.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuipongeza UWT kwa wazo  zuri walilokuja nalo na pia kushirikiana na Jumuiya zote za CCM kufanikisha jambo hilo kwa msingi kuwa ni lao wote.

Mapema uongozi wa UWT ulimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa juhudi kubwa anazozichukua katika uongozi wake sambamba na kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi hasa uchumi wa Buluu katika uongozi wake kama Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 ilivyoelekeza

Kitengo cha habari,

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.