Habari za Punde

Wakulima wa Zao la Mkonge Mkoani Tanga Ruksa Kumiliki Mashine za Kuchakata Mkonge katika AMCOS Zao.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya mkonge nchini Saad Kambona akiongea na wajumbe ambao ni viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) wilayani Korogwe.

Mwenyekiti wa Wenyeviti  wa Amcos mkoani Tanga Grayson Mnyari akiongea akiongea  na wajumbe wakati wa kikao hicho.

Wenyeviti wa AMCOS za Wilaya ya Korogwe wakifuatilia kikao hicho, wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa Magunga Amcos Shedrack Mbwambo.
Baadhi ya Wajumbe na watumishi wa Taasisi za fedha walioalikwa wakifuatilia mada za viongozi.

Na Hamida Kamchalla 

Bodi ya Mkonge nchini imetoa ruksa kwa wakulima wa mkonge kumiliki mashine za kuchakata mkonge kwa madai kwamba Wasimamizi wao ambao ni Kampuni ya Sisalana kushindwa kukidhi mahitaji yao.

Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge nchini Saad Kambona amesema muafaka huo umetokana na malalamiko ya wakulima anayopata ambapo pia kwa ajili ya kunusuru pato la Taifa kutokana na kupata hasara za mazao hayo kukauka kwa kukaa kiwandani bila kuchakatwa inapotokea mashine ya kuchakatia kuharibika.

Wakulima na wenyeviti wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wamesema taasisi hiyo inavyoelekea haina uwezo wa kuendesha shuhuli ambayo wanaifanya kutokana na kuharibikiwa kwa mashine za korona mara kwa mara na kusababisha mazao yao kukauka wakati yakiwa kiwandani kabla ya kuchakatwa.

Kampuni tanzu ya NSSF inayojulikana kama Sisalana inakabiliwa na changamoto la kuharibika kwa mashine ambazo ni za muda mrefu jambo linalopelekea kutowatimizia wateja wao mahitaji lakini pia kukiuka sheria za mikataba yao.

Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ina jumla ya Amcos 5 za kilimo cha zao la kimkakati la Mkonge ambazo ni Magunga, Mwelya, Mgombezi, Hale pamoja na Magoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.