Habari za Punde

Zanzibar yafikiria jinsi ya kuitumia safarafu ya Kidijitali ( Digital Currency)

Na Sharifa Maulid

 Waziri wa nchi afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakaa pamoja na wa safarafu ya kidigitali(Digital currency)  ili kuona kwa namna gani Zanzibar itaweza kuitumia sarafu hiyo.

Waziri Soraga ameyasema hayo ofisi kwake Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B Unguja wakati alipokutana na viongozi wa kampuni ya Hypertech Company limited kutoka nchini South Africa, ili kujadili namna ya kuitambulisha sarafu ya kidigali kwa ndani ya Zanzibar.

Akiwasilisha kwa Mhe Waziri juu namna dunia inavyotumia sarafu hiyo mwakilishi wa biashara hiyo Mr. Joe Chuene amesema muelekeo wa dunia sasa ni kutumia sarafu ya kidigitali kufanya manunuzi ya vitu mbali mbali na kwasasa sarafu hiyo inatumiwa na watu mbali mbali pamoja na makampuni makubwa kote duniani.

Aidha ameongeza kuwa kwa sasa mzunguko wa sarafu ya kidigitali(Digital Currency) umefikiwa kiwango cha fedha 3.2 trillion duniani kote, hivyo ameiyomba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuitambulisha sarafu hiyo kwa wananchi ili iweze kutumika kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi na serikali kwa ujumla

Akifunga mjadala huo Mhe Soraga amewahakikishia viongozi hao kuwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar italichukulia suala hilo kwa umuhimu mkubwa ili kuona kwa jinsi gani jambo hilo linaweza kufanikiwa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.