Habari za Punde

Mama Mariam Mwinyi kuwaunga mkono vijana kusukuma mbele maendeleo

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akizungumza kupitia njia ya mtandao  katika Mkutano Mkuu wa Vijana Kivuli wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021,uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdul Wakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, kwa mara ya kwanza wenye sura ya Kimataifa, wenye kauli mbiu “Fursa na Uwekezaji wa Vijana katika Uchumi wa Buluu”.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu Kivuli wa Vijana wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akizungumza kupitia kwa njia ya mtandao (hayupo pichani) mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, na kuwashirikisha Vijana mbalimbali, ukiwa na kauli mbiu “Fursa na Uwekezaji kwa Vijana katika Uchumi wa Buluu”.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Vijana Kivuli wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza kwa njia ya mtandao, katika mkutano wa Mkuu Kivuli wa Vijana wa Umoja wa Mataifa, kwa mara ya kwanza wenye sura ya Kimataifa, uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Mkutano Mkuu wa Vijana Kivuli wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021, Ndg. Ahmada Salum Suleiman akiongoza Mkutano huo uliofanyika  katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, unaozungumza Uchumi wa Buluu, ukiwa na kauli mbiu “Fursa na Uwekezaji wa Vijana katika Uchumi wa Buluu”.(Picha na Ikulu)
MJUMBE wa Mkutano Mkuu Kivuli wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021, Mwakilishi kutoka Canada  Ndg.Adil Ali Bakari, akichangia wakati wa mkutano huo wa Vijana uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, ukiwa na kauli mbiu “Fursa na Uwekezaji wa Vijana katika Uchumi wa Buluu”(Picha na Ikulu)
MWAKILISHI kutoka Nchini Australia Ndg.Abdulsamad .M.Suleiman akijubu hija zilizoibuliwa na Wajumbe wa mkutano wa kwanza wenye sura ya Kimataifa Kivuli wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021, uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amewahakikishia vijana kwamba ataendelea kuwaunga mkono katika kusukuma mbele maendeleo endelevu.

Mama Mariam Mwinyi ameyaswema hayo leo wakati akitoa salamu zake kupitia mtandao katika mkutano wa Vijana Kivuli wa Umoja wa Mataifa Zanzibar unaofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni Zanzibar.

Katika salamu zake hizo, Mama Mariam Mwinyi alisema kuwa milango ya ofisi yake iko wazi na kuwanasihi vijana kutoa mawazo dhidi ya vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake.

Alisema kuwa anatambua kwamba kuna changamoto nyingi zinazowadhalilisha na zinazowarudisha nyuma wanawake na vijana wa kike na kutoa wito kwa vijana hao kuendelea kuyazungumza masuala hayo.

Pia, Mama Mariam Mwinyi aliwasihi vijana wa kike kushiriki kikamilifu na kutoa mawazo yao yatakayoleta mabadiliko chanya yenye kuakisi maendeleo ya wanawake.

Alieleza kuvutiwa na kauli mbiu ya mkutano huo isemayo “Fursa na Uwekezaji wa Vijana katika Uchumi wa Buluu”.

Hivyo, alieleza matarajio yake kwamba mkutano huo utajadili masuala muhimu yenye kuhusu Sera ya Uchumi wa Buluu, mchango wa vijana katika kushiriki uchumi huo, na kuyaweka pamoja mawazo yao kwa lengo la kuishauri Serikali.

Aidha, Mama Maria Mwinyi alieleza kwamba maamuzi ya kukusanyika vijana pamoja na kujadili masuala mbali mbali kwa ajili ya Maendeleo yao na ya Taifa lao ni jambo muhimu “Hakika mmefanya jambo kubwa sana linalostahili pongezi”,alisema.

Sambamba na hayo, Mama Mariam Mwinyi aliwapongeza vijana wote kwa ujumla wao baada ya kutafsiri kwa vitendo mawazo yao na kuandaa mkutano huo kwa mara ya kwanza wenye sura ya Kimataifa. “Hakika hii ni fursa kubwa kwa nchi yetu na kwa vijana wote wa Taifa Letu”,alisisitiza Mama Mariam Mwinyi.

Imetayarishwa na Kitengo cha Mawasiliano

Ikulu Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.