Habari za Punde

Serikali Imejipanga Vema Katika Kuwawezesha Vijana Kiuchumi.

Na.Mwandishi Wetu.

Waziri wa habari, vijana,  utamaduni, sanaa na michezo  Tabia Maulid Mwita amesema  Serikali imejipanga vyema katika kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuanzisha mpango wa ajira kwa vijana ambao utawasaidia vijana kupata fursa za kimaendeleo.

Amesema hayo wakati wa kuzindua mkutano wa kwanza wa Jumuiya ya vijana wa umoja wa kitaifa Zanzibar katika ukumbi wa Idriss Aabdulwakil kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi. Kuahidi kupokea mapendekezo yatakayotolewa na vijana katikamkutano huo pamoja  na kuyafanyia kazi. kwani yana lengo la
kuleta maendeleo na mabadiliko katika nchi yetu.

Mhe Tabia amewataka vijana kutokata tamaa kwani wanauwezo mkubwa wakuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika nchi.

Aidha amewataka vijana kuzitumia fursa zinazotolewa katika kuhakikishawa na kujiletea maendeleo kwao na taifa kwa ujumla  kwani Serikali inalengo la kuwasaidia vijana wote ili kuwa wachapakazi wazuri na kuweza kujitegemea wenyewe.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka  amesema shughulihiyo  iliyoandaliwa na vijana  ina umuhimu mkubwa wa kuleta  maendeleoya vijana kwa kupata fursa nyingi katika jamii na kuchangia maendeleo ya nchi .

Menu elk to wa mkutano huo  Ahmada Salum Suleiman amesema lengo la mkutano huo  ni  kuwakusanya vijana kutoka mataifa mbalimbali kujadili nafasi za vijana na uwekezaji wa uchumi wa buluu  ili kuleta azimiokuu  la vijana kwa mwaka 2021.

Mratibu wa shirika la umoja wa mataifa Zanzibar Nd. Dorothy Temuusiri amesema kuwa  huo ni muendelezo wa kuwahusisha vijana katika kuzungumzia matatizo yao pamoja na kuchangia mawazo yao katika kuisaidia nchi  katika masuala ya kimaendeleo ikiwa ni miongoni mwafursa zitakazowasaidia .

Muhamasishaji Adil Ali Bakari  ameeleza kua kongamano hilo hutoa fursa za kuengeza uelewa kwa vijana   na kutoa michango itakayoshawishi Serikali katika utekelezaji wake wa kuleta maendeleo katika  nchi.

Mkutamo huo ni mkutano kivuli mkuu wa umoja wa mataifa ambao ni wa kwanza kwa upande wa Zanzibar uliowajumuisha vijana kutoka nchi mbalimbali za umoja wa kimataifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.