Habari za Punde

Maradhi yasiyoambukiza yaweza kuongezeka kama hatutobadilisha mfumo wa vyakula

 NA Khadija Khamis – Maelezo , 21 / 12/2021

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Maradhi Yasioambukiza Zanzibar (ZNCDA) Said Gharib Bilali amewataka wadau wa maradhi yasioambukiza kwa kujenga uelewa wa kukabiliana nayo pamoja na kutoa elimu kwa wengine ili kupunguza ongezeko la waathirika.

Akiyasema hayo katika  ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Magufuli Mwanakwerekwe wakati wa Mkutano wa siku moja kwa wadau wa maradhi yasioambukiza.

Amesema maradhi hayo hayaambukizi lakini yanavishawishi vingi hatarishi ambavyo hupelekea kuingia katika hatari ikiwemo mfumo wa vyakula vinavyotumika katika jamii.

Aidha alisema jamii kukosa uelewa wa vyanzo na visababishi vinavyopelekea maradhi hayo  huchangia ongezeko  .

Nae Muasilishaji Mada, Mkuu wa Kitengo cha Maradhi yasiambukiza Mnazimmoja Omar Abdalla Ali alisema maradhi yasioambukiza hayana dalili wala ishara za haraka zinamuonyesha mtu kujigundua mapema  

Alifahamisha kuwa jamii iweke mikakati ya kukabiliana na maradhi hayo ikiwemo kuchukuwa tahadhari katika visababishi hatari  vya maradhi hayo .

Alifahamisha maradhi yasiambukiza yanayoongoza ni  shindikizo la damu,(Presha) ajali za barabarani, kisukari, saratani ya shingo ya kizazi, tenzi dume, matatizo ya meno pamoja na afya ya akili .

 Alieleza suala la elimu kwa wafanyakazi  wa afya linahitajika jambo ambalo litasaidia kuokoa wagonjwa wa presha na sukari kupoteza maisha .

“Wafanyakazi wanahitajika kupewa elimu ya kutosha ili kukabiliana na jamii kwa ushauri nasaha na kuwapa uelewa wa matumizi ya dawa kwa wagonjwa na mfumo bora wa ulaji .”alisema Mkuu wa Kitengo .

Nao Wadau wa maradhi hayo Wamesema  mpango maalum unahitajika wa kudhibiti ajali za barabarani ambazo zinaongezeka siku hadi siku jambo ambalo linachangia ulemavu wa kudumu na kupoteza uhai wa  watu wengi .

Wamewataka wadereva, wenye vyombo vya maringi mawili pamoja na waendao kwa miguu  kuwa makini katika matumizi ya barabara  kwa kutii sheria za usalama ili kuepusha ajali .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.