Habari za Punde

Mkoa wa Tanga Waomba Kuharakishwa kwa Ujenzi wa Barabara ili Kupunguza Msongamano Bandari ya Dar.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Godfrey Kasekenya akizungumza na wafanyakazi wa TANROADS wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 16 wa Baraza la Wafanyakazi Tanroads uliofanyika Mkoani Tanga.
Baadhi ya Wafanyakazi wa TANROADS wakimsikiliza Naibu Waziri wakati akifungua mkutano.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya kushoto akiteta jambo na mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa kabla ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa 16 wa wafanyakazi wa Bodi ya Barabara nchini (TANROADS) uliofanyika jijini Tanga.

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ameomba kuharakishwa kwa ujenzi wa barabara yenye urefu wa takribani km 400 ambayo itarahisisha usafiri na kupanua wigo wa biashara ndani ya Mkoa huo na nchi jirani ili kufupisha umbali kwa watumiaji wa bandari ya Tanga wa nchi za jirani.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa alitoa ombi hilo leo kwa niaba mkuu wa mkoa, wakati akimkarihisha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya, kwenye mkutano wa 16 wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS, jijini hapa 

Mgandilwa alisema upanuzu wa bandari ya Tanga utachochea kasi ya maendeleo kwa Mkoa na kwa Taifa lakini ipo haja ya kuharakisha ujenzi wa barabara inayotokea Handeni kupitia Wilaya ya Kilindi hadi mkoani Manyara katika Wilaya ya Kiteto hadi Kondoa ambayo itarahisisha usafiri kwa wasafirishaji.

"Muheshimiwa, upanuzi wa bandari hapa, unafanya Tanga kukua kiuchumi, na sasa tunaona kwamba nchi jirani ndio wanaitumia sana bandari yetu wakiongozwa na nchi ya Rwanda, kunaa kiwanda kimoja Cha kutengeneza saruji Rwanda malighafi yao wanaipitishia hapa, mzunguuko wake kutoka hapa ni mpaka kwao ni umbali mrefu sana" alisema.

"Hivyo nikuombe muheshimiwa, kuna barabara moja ambayo tunaweza tukaioasua hapo katikakati ya kutoka Handeni - Kibirashi kutokezea Kiteto kwenda Kondoa, hii barabara ina urefu wa kama km 400, tukiipasua hii barabara tunaweza tukapunguza msongamano mkubwa wa magari ya Rwanda yanayokwenda kuchukua mizigo kwenye bandari ya Dar es salaam na badala yake waje wachukulie hapa" aliongeza.

Kufuatia hilo Mgandilwa alisisitiza "kwahiyo nikuombe muheshimiwa Naibu Waziri uongee na Mameneja wa Mikoa miwili au mitatu inayopita barabara hiyo, tulibebe hili kwa uzito ili mwisho wa siku tuweze kuondoa msongamano uliopo bandari ya Dar es salaam na kutengeneza fursa katika bandari zingine ambazo zipo na serikali inazitekeleza kwa kiwango kikubwa".

Hata hivyo alifafanua kwamba kumekuwa na tatizo la mahusiano kati ya viongozi wa Mikoa hususani kwa Mameneja na wakuu wa Mikoa ambapo Mgandilwa aliwakumbusha kukaa pamoja na kuongea matatizo yao pindi yanapowatokea na kutafuta suluhisho badala ya kupeana maneno yasiyi ya kimaadili ya kazi.

"Najua hiki kikao ni cha Baraza la Wafanyakazi, wapo wafanyakazi wa kawaida lakini wapo Mameneja wa mikoa, wakati mwengine kumekuwa na changamoto ya mahusiano sana kati ya Mameneja wa Mikoa na viongozi wao wakuu wa Mikoa kwenye maeneo yao husika na huwa wanawekwa pamoja kwenye kikao kimoja tu cha Ushauri wa Bodi ya Barabara" alifafanua.

"Niwaombe kuwakumbusha, viongozi kwenye Mikoa yenu ni wakuu wa Mikoa, ni vema mkaboresha mahusiano yenu katika maeneo yenu siyo tu kwenye vikao vya roadbord, kuna suala lolote ni vema mkaenda mkakaa na kiongozi mkajadiliana mwisho wa siku mtaweza kupata muafaka na siyo kukaa na kupiga maneno ya siasa na kiutendaji" aliomba Mgandilwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.