MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk
Khatib, akizungumza na wananchi wa mkoa huo, huko Wilaya ya Micheweni mara
baada ya kumalizika kwa zoezi la ufanyaji wa usafi wa mazingira, ikiwa ni
shamrashamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MBUNGE wa Jimbo la Tumbe Amour Khamis Mbarouk
akifagia katika majani huko Micheweni wakati wa usafi wa mazingira, ikiwa ni
shamrashamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya,
akitia taka katika bero maalumu kwa ajili ya kwenda kutupwa wakati wa ufanyaji
wa usafi huko Micheweni, ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 58 ya
Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali,
akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Chake Chake walioshiriki katika usafi wa
Mazingira katika barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa Pemba, ikiwa ni
shamrashamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya zanzibar.(PICHA NA HANIFA SALIM, PEMBA)
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali,
akikata majani katika eneo la Mabaoni Wilaya ya Chake Chake wakati wa usafi wa
mazingira ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi
matukufu ya Zanzibar.(PICHA NA HANIFA
SALIM, PEMBA)
No comments:
Post a Comment