Habari za Punde

Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kiwanda cha bomba za Plastiki cha Kasu Industrial

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh.Simai Mohammed Said akifungua pazia kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi katika kiwanda cha  bomba za plastiki cha Kasu Inderstrial CO.LTD kilichopo Maruhubi   kuelekea maadhimisho ya  miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh.Simai Mohammed Said akihutubia katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kiwanda cha  bomba za plastiki cha Kasu Industrial CO.LTD kilichopo Maruhubi   kuelekea maadhimisho ya  miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Picha na Fauzia Mussa –Maelezo Zanzibar.

Na Rahma Khamis, Maelezo.  1/1/2022

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohd  Said amewataka vijana watakaobahatika kupata fursa za ajira katika kiwanda cha mabomba ya plastiki (KASU INDUSTRIAL LTD) ,kitakapomalizika  kufanyakazi kwa bidii na maarifa huku wakielewa kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kuleta mafanikio binafsi na Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho huko Maruhubi Mjini Unguja ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 58 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Amesema kuwa kuwa eneo la Maruhubi lilijulikana kuwa ni eneo la viwanda na wakati huo viwanda kadhaa vilijengwa katika ukanda huo mara baada ya mapinduzi ya mwaka 1964.

Adha amefahamisha kuwa viwanda hivyo vilifanyakazikwa ufanisi mkubwa hadi pale palipotokea mabadiliko ya kiteknolojia ulimwenguni ambapo viwanda hivyo vilishindwa kukabiliana na mabadiliko hayo na kuanza kushindwa kuzalisha kwa faida na kupelekea kufungwa kimoja baada ya kimoja.

Waziri Simai amesema kuwa miongoni mwa viwanda vilivyoshamiri katika miaka hiyo katika eneo hilo ni kiwanda cha sigara(Tabia Njema) kiwanda changozi na viatu(Mwendo)kiwanda cha maziwa na kiwanda cha chakula cha mifugoa, pamoja na kiwanda cha nguo cha cotex.

  Aidha ameeleza kuwa katika nchi zilizoendelea zimekuwa zikifanya jitihada mbalimbali ambazo zinaweza kupatikana kadri sekta inapoimarika ikiwemo fursa za ajira kwa wananchi, kuchangia pato la taifa kupitia kodi na tozo mbalimali ili kupunguza wa uagizaji wa bidhaa kutoka nje.

Akitoa maelazo mafupi kuhusu ujenzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Islam Seif amesema kuwa mradi huo umeanza mwaka 2016 na wawekezaji wazalendo na kuunga mkono azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema kuwa kuwa wanatarajia kua wanufaika wa kiwanda hicho ni wananchi wazalendo na kitakapokamilika kina uwezo wa kuzalisha na kuuzwa katika masoko ya Zanzibar na nchi jirani .Aidha amefahamisha kuwa kiwanda hicho kinatumia vitu vya plastiki hivyo itarahisisha kuondosha takataka za plastic na kuzitumia kama malighafi.

Nae muwekezaji wa kiwanda hicho Hussein Kassu  amesema kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni baada ya kuona kuwaa  kuna haja kubwa ya kuzalisha bidhaa hizo ili kurahisisha upatikanaji wa soko hapa  nchini.

Amesema kuwa katika kuleta jitihada za kuwapatia ajira vijana wameamua kujenga kiwanda hicho kubainisha kuwa ni salama kwa wananchi  na mazingira yaliyopo kwani hakizalishi kemikali yeyote ya aina ya uchafu wa mazingira.

Aidha amefahamisha kuwa gharma za tozo za umeme ni kubwa  pamoja na kukatika kwa umeme mara kwa mara jambo ambalo linawatia hofu  ya kupanda kwa gharama  zaidi baada ya kuanza kufanya kazi kwa kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.