Habari za Punde

Maziko ya Askofu Mstaafu Dkt.Gerald Mpango Kasulu Mkoani Kigoma.

 

Kwaya ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika wakiimba wimbo wa maombolezo wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Gerald Mpango iliofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea wilayani Kasulu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akitoa neno la shukrani kwa waombolezaji mbalimbali waliojitokeza katika ibada ya mazishi ya kaka yake aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Gerald Mpango iliofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea wilayani Kasulu. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akitoa neno la shukrani kwa waombolezaji mbalimbali waliojitokeza katika ibada ya mazishi ya kaka yake aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Gerald Mpango iliofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea wilayani Kasulu. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango pamoja na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiweka shada la Maua katika kaburi la aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Gerald Mpango wakati wa mazishi yaliofanyika katika kanisa la Anglikana la  Mtakatifu Andrea  lililopo Kasulu Mkoani Kigoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Gerald Mpango iliofanyika katika kanisa la Anglikana la  Mtakatifu Andrea  lililopo Kasulu Mkoani Kigoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  akiweka mchanga katika kaburi la  aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Gerald Mpango wakati wa mazishi ya Askofu huyo yaliofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea wilayani Kasulu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akitoa heshima za mwisho katika mwili wa kaka yake aliyekuwa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Askofu Gerald Mpango wakati wa ibada ya mazishi iliofanyika katika kanisa la Anglikana la  Mtakatifu Andrea  lililopo Kaulu Mkoani Kigoma. Januari 22,2022.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa leo tarehe 22 Januari 2022 ameongoza waombolezaji katika mazishi ya kaka wa Makamu wa Rais na Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dkt. Gerald Mpango  yaliofanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Askofu Mpango alifariki dunia tarehe 19 Januari 2022 jijini Dar es salaam.

Ibada ya Mazishi imefanyika katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea Kasulu mkoani Kigoma ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Askofu Maimbo Mndolwa. Akizungumza wakati wa mahubiri Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Donald Mtetemela amemtaja Askofu Mpango kama kiongozi aliyempenda Mungu. Amesema alikuwa na moyo wa uinjilisti na alihubiri ndani na nje ya nchi na mara zote aliongoza ujenzi wa Makanisa ili kuendelea kuhubiri injili.

Askofu mstaafu Mtetemela amesema Askofu Mpango alichukia umasikini na aliipenda nchi yake. Amesema aliwasaidia wakimbizi pamoja na kuchagiza kuletwa kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi (UN HABITAT) mkoani Kigoma lililosaidia wengi.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msaada wa rambirambi  pamoja na neno la faraja katika kipindi cha msiba huo. Makamu wa Rais amesema anashukuru kwa faraja aliopata kutoka viongozi mbalimbali kutoka serikalini pamoja na wastaafu, kutoka katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa vyama vya siasa, Mabalozi kutoka nchi mbalimbali, viongozi wa dini pamoja na taasisi mbalimbali.

Makamu wa Rais amesema ukoo umepata pigo kwa  kuondokewa na kiongozi wao aliyekuwa chachu ya kuwaunganisha na kuwasaidia wakati wote. Amesema familia imempoteza mtu aliyekuwa na huruma na alipenda elimu na kuwahamasisha kushika elimu wakati wote.

Akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema serikali imepoteza kiongozi wa dini aliyekuwa na mchango mkubwa katika taifa. Waziri Mkuu amasema jamii ina jukumu la kuyaenzi  na kuyaendeleza mema yote alioyafanya askofu Mpango enzi za uhai wake ili yaendelee kuleta manufaa katika jamii.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa dini katika kuimarisha Amani, umoja na mshikamano hapa nchini. Aidha amesema serikali itaendelea kuunga mkono katika uendeshaji wa dini na uhuru wa kuabudu katika dini yeyote ile utaendelea kulindwa.  Waziri Mkuu amewaasa viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa i ili Tanzania iendelee kuwa kitovu cha Amani duniani.

Mazishi ya Askofu Mpango yamehudhuriwa na Mawaziri pamoja na Manaibu Mawaziri  Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Katanga, Wakuu wa Mikoa , Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Viongozi wa vyama vya siasa, wananchi wa Kigoma na maeneo jirani, Maaskofu wa kanisa la Anglikana na Viongozi wa dini mbalimbali.

Mwili wa Askofu Gerald Mpango umezikwa katika viunga vya kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea lililopo Kasulu Mkoani Kigoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.