Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi akutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipofika Ikulu Jijiji Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu  leo 8-1-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa wakiangalia mandhari ya  bahari, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 8-1-2022.(Picha na Ikulu)

/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 8-1-2022.(Picha na Ikulu)  
 

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

 Zanzibar                                                                                                08.01.2022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa pongezi kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika vikao vya Muungano ikiwa ni pamoja na kutatuliwa mambo kadhaa. 

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa na kumpongeza kwa kumtembelea.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi kwa usimamizi mzuri wa vikao hivyo vya Muungano ambavyo vimeweza kuleta tijao na kutatua mambo kadhaa ambapo kati ya Hoja 18 tayari Hoja 11 zimeshapatiwa ufumbuzi na kwa zile zilizobaki ufumbuzi wake utapatikana ndani ya muda mfupi ujao. 


Rais Dk. Mwinyi alitoa salamu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mashirikiano mazuri yaliyopo hatua ambayo imekuwa na maslahi mazuri kwa pande zote mbili ikiwa ni pamoja na mgao wa fedha za mkopo wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), hatua ambayo itasaidia kujenga huduma za jamii pamoja na kuwapangia mipango wajasiriamali.


Alisema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa na msaada mkubwa katika kuimarisha uchumi wa Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeridhika na hatua ya mashirikiano inavyokwenda hali ambayo itasaidia kuimarisha na kukuza uchumi kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Rais Dk. Mwinyi alitoa shukurani kutokana na nchi kuwa na amani na utulivu na kusema kwamba hatua hiyo ndio inayopelekea kuimarika kwa uchumi na kueleza kwamba kwa upande wa Zanzibar, utulivu umeweza kupatikana na wananchi wanashirikiana vyema na hivi sasa kuna kila sababu ya kupiga hatua kimaendeleo.


Alieleza athari za UVIKO -19 zilivyoathiri uchumi wa Zanzibar na kueleza jinsi  dalili za kuongezeka kwa watalii na kueleza haja ya Zanzibar kujifunza katika ukusanyaji wa mapato hasa baada ya janga hilo la maradhi kutokana na uchumi wa Zanzibar kuwa tegemezi kwa utalii.


Nae Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa  alitoa pongezi kwa Rais Dk. Mwinyi kwa kupata fursa ya kuiongoza Zanzibar hali ambayo anastahili na ameanza vizuri kuongoza kwani nchi imetulia na mahusiano ya Wazanzibari yamezidi kuimarika.


Alipongeza kwa jiansi ya Rais Dk. Miwnyi wanavyoshirikiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanioa Mama Samia Suluhu Hassan na kuahidi kwa upande woa wasaidizi kuahidi kupokea maelekezo  yao na kusimamia majukumu ya kuwatumia Watazania wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Alitumua fursa hiyo kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa jitihada zake za kuimarisha uchumi na hasa katika kuitumia fursa ya Uchumi wa Buluu ambao ni uchumi wa Buluu na kuweka nguvu katika uchumi huo na kueleza kwamba kwa upande wa Tanzania Bara nayo itapanua wigo kutokana na Sera hiyo aliyoiweka Dk. Mwinyi katika uchumi. 


Waziri Majaliwa alimuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kwamba juhudi za makusudi zitaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha vikao vya Muungano vinaleta tija na kuweza kuondoa changamoto zilizopo kwa haraka.

Alimuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kwamba mamla za ukusanyaji wa kodi zitahakikisha zinakusanya kodi bila ya kutumia nguvu kwa lengo la kuwajengea imani Watanzania kwa Serikali yao pamoja na kuwaamini viongozi wao wote ili nchi izidi kupata mafanikio.

Mapema, Rais Dk. Mwinyi alifanya mazungumzo na   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anayeshughulikia Masuala ya Watu wenye Ulemavu Ummi Khamis Nderiananga Ikulu Zanzibar na kueleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inawasaidia watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwajenga vyuo vya amali Unguja na Pemba ili wapate elimu za stadi za maisha.

Rais Dk. Mwinyi alisisitiza kwamba unapotaka kumuwezesha mtu ni vyema ukampa elimu kwanza ili iweze kumsaidia katika kuendesha shughuli zake na ndio maana Serikali imeamua kuchukua hatua hiyo ya kutaka kuwajengea vyuo wajasiriamali.

Katika maelezo hayo Rais Dk. Mwinyi alisisitiza kwamba Serikali zote mbili ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafanya kila iwezekanavyo katika kuhakikisha inawasaidia na inawaunga mkono watu wenye ulemavu.

Alifahamisha kwamba miongoni mwa mikakati na azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwasaidia watu wenye ulemavu ni kuhakikisha fedha za mkopo wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambapo wajasiriamali watasaidiwa pia, watu wenye ulemavu nao watafaidika na fedha hizo ili kuwaondoa katika dimbwi la umasikini.


Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameleza uwepo wa watu wenye ulemavu ndani ya Serikalini na kusisitiza haja ya kuongezeka kwa idadi yao huku akieleza kwamba wazo la kuwasaidia watu wenye ulemavu mmoja mmoja nalo litafanyiwa kazi ili mafanikio yaweze kupatikana kama vile yalivyopatikana kwa upande wa Tanzania Bara.


Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kumpongeza Naibu Waziri Ummi Nderiananga kwa ziara yake aliyoifanya Unguja na Pemba sambamba na kuendeleza mashirikiano zaidi kati ya Serikali zote mbili hasa  katika wakati huu wa shamrashamra za miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Januari 1964.


Nae Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anayeshughulikia Masuala ya Watu wenye Ulemavu Ummi Khamis Nderiananga alieleza salamu za watu wenye ulemavu alizopewa ili azifikishe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Alitoa pongezi kwa hatua za uteuzi ambazo amezifanya Rais Dk. Mwinyi kwa watu wenye ulemavu ambapo pia, wakuu wa Mikoa nao wamemuunga mkono juhudi hizo kwa kuwateua Masheha ambao ni watu wenye ulemavu huku akieleza kwamba Serikali zote mbili zilivyoweka mikakati ya kuwasaidia watu wenye ulemavu.

Aidha, Naibu Waziri Ummi Nderiananga amewaeleza watanzania wote kuwa Serikali zipo imara katika kuwasaidia na kuwashirikisha watu wenye uleamvu katika masuala mbalimbali. 

Imetayarishwa na kitengo cha Habari

Ikulu Zanzibar


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.