Habari za Punde

Mfahamu Mchezaji Gwiji Zanzibar Abdulwakati Juma Mchezaji wa Timu ya Small Simba na Timu ya Taifa.


Anaitwa Abdallah Juma Alley ila wengi humwita AbdulWakati Juma. Mzaliwa wa Zanzibar 1959 akiwa ni mmoja kati ya watoto  wa aliekuwa Waziri wa Fedha wa Zanzibar Juma Alley. Mchezaji wa Taifa ya Tanzania wa michezo miwili(soka na table tennis) na pia mchezaji wa kwanza kama sio pekee Afrika Mashariki kuchezea timu mbili tofauti za taifa. Mataifa hayo ni Tanzania na Oman.

Alipewa jina la Abdulwakati ikiwa ni njia ya kuwatofautisha Abdul watatu waliopatikana katika timu ya Hero Boys. Kwa kuwa  alicheza kiungo wa kati likuwa rahisi  kupewa jina la Abdul-wa-kati. Akiwa na miaka 13 alijiunga na timu ya Small Simba  alikodumu kwa miaka 8 ambapo sio tu aliisaidia timu hiyo kupanda daraja lakini pia alichaguliwa timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar. 

1984 alishiriki katika kombe la Challenge na timu ya Zanzibar lililofanyika Mombasa ambako alikutana pia na  mawakala kutoka Oman ambao baada ya kufurahia uchezaji wake walimchukuwa Oman ili akachezee timu ya taifa ya huko. Akiwa  Oman alifanikiwa kuifikisha nafasi ya nne  katika kombe la Ghuba akiwa yeye ni mmoja kati ya walioifunga timu ya Qatar mabao 2-1.

Kwa upande wa table tennis(Mpira wa Meza) amekuwa  bingwa wa mchezo huo kwa miaka 4 mfulilizo(kombe la Costal Town Championship) Amecheza All Africa Games yaliyofanyika Misri na Algeria baina ya 1977-1978 ambapo walifanikiwa kufika robo fainali ya mashindano hayo.

Abdulwakati ni mtanzania wa kwanza kucheza soka Oman katika timu ya Taifa. Hajawahi kupoteza mchezo wowote wa tennis kwa timu za Tanzania mpaka anastaafu mwaka 1978. Amefungua njia kwa soka la kulipwa kwa watanzania, ameipatia timu ya Fanja Oman medali 8 za dhahabu, amepata mafunzo ya soka kutoka  France, Brazil, Malaysia na nchi zote za Ghuba. amefundishwa kocha Omar Boras(alieifundisha Uruguay kombe la dunia  1986).

Abdulwakati kwa sasa ni mwajiriwa wa Kiwanja cha kimataifa cha ndege Abeid Amani Karume katika kampuni ya Transworld. 

Ushauri wake kwa vijana...wacheze kwa juhudi kwani mpira sasa ni biashara.

Abdulwakati Juma ni Hazina kutoka Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.