Habari za Punde

Rais Mhe. Samia, ashiriki katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi nchini kilichofanyika Jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi nchini leo tarehe 08 Februari, 2022. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla

 

Wakuu wa Mikoa, Mawaziri pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwa katika Kikao Kazi cha Wakuu hao wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 08 Februari, 2022.

Wakuu wa Mikoa, Mawaziri pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwa katika Kikao Kazi cha Wakuu hao wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 08 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Kikao cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Mawaziri pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakati wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea kwa niaba yake Bango lenye wa Anwani ya Makazi ya Ofisi ya Rais, Ikulu mara baada ya kuzungumza katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa

kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.