Na Happiness Shayo-WMU
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani pamoja na kuadhimisha miaka 45 ya
Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza katika ziara hiyo, Naib u Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewapongeza UWT Taifa kwa kufanya
ziara hiyo.
“Kwa hiki kitendo mlichokifanya mmekuwa
mabalozi wakubwa ambao tunategemea mtaleta makundi mengine kutembelea hifadhi
zetu na maeneo mengine yaliyo na vivutio Tanzania nzima ” Mhe. Masanja amesema.
Amesema kupitia utalii wa ndani Tanzania
inatangazwa ndani na nje ya nchi lakini pia watalii wanachangia katika pato la
Taifa.
Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kutangaza
utalii.
“Kipekee namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kiungo katika kuhamasisha Utalii
wa ndani lakini pia naushukuru uongozi wa UWT Taifa na washiriki wote kwa
kumuunga mkono Mhe. Rais kuja kutembelea Hifadhi yetu ya Serengeti.”
Katika kuendeleza kutangaza utalii wa ndani,
Mhe. Masanja amesema kuelekea Maadhimisho
ya Siku ya wanawake duniani atahamasisha wanawake nchi nzima kutembelea kivutio
cha utalii kilicho katika maeneo wanayoishi ili kutangaza utalii wa ndani.
Naye, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudensia Kabaka
ameahidi kwamba UWT itakuwa balozi katika kutangaza utalii wa ndani.
“Sisi tutakuwa mabalozi wa utalii wa ndani
tukimuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan na kuongeza kuwa furaha yake ni kuona kwamba wanahamasisha utalii wa
ndani kupitia wanawake zaidi ya 100 waliotoka katika mikoa yote nchini
Tanzania.
Amesema watahamasisha makundi mengine
kutembelea mbuga za wanyama ili kuchangia pato la Taifa.
Amewataka Watanzania kubadili fikra za kuona
kwamba wazungu ndio wanaoweza kuingiza fedha katika Sekta ya Utalii na badala
yake wabadilike kwa kuwa wazalendo kutembelea vivutio vya utalii ili kuchangia
pato la Taifa.
Katika hatua nyingine, katika ziara hiyo umezinduliwa utalii wa michezo ambao pamoja na mambo mengine watalii watakaotembelea hifadhini watapata fursa ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama kuvuta kamba, netball, kukimbia na magunia n.k.
No comments:
Post a Comment