Habari za Punde

Wakala wa Mbegu za Kilimo Nchini ASA Waja na Mwarubaini wa Kuondoa Tatizo la Uhaba wa Mafuta Nchini.

MKUU wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu katika akimkabidhi miche ya michikichi 30,000 Mkuu wa Kitengo cha Mazingira (Dawasa) Mhandisi Modester Mushi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kando kando ya Mto Ruvu na kuwaongezea wananchi kipato ambapo miche hiyo ilitolewa na Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA)kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo

NA OSCAR ASSENGA,MKINGA.

WAKALA wa Mbegu za Kilimo Tanzania (ASA) umesema kwamba lengo lao kubwa hivi sasa ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa mafuta linapungua nchini kwa kutumia zao la mchikichi ambalo ni zao la kimkakati kwa kuzalisha mafuta.

Hatua hiyo inatajwa kwamba itapunguza gharama kubwa ambazo Taifa linaingia kuagiza mafuta kutoka nje na hivyo kuondokana na adha ya kutumia fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya bidhaa hiyo.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo wakati wa halfa ya makabidhiano ya Mbegu za Michikichi 30,000 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa)kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kando kando ya Mto Ruvu na kuwaongezea wananchi kipato

Halfa hiyo ilifanyika kwenye Shamba la Mwele lililopo kata ya Maramba wilayani Mkinga ambalo limepewa jukumu la kuzalisha mbegu za michikichi, Miche hiyo ilitolewa na Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA)

Alisema mbali na michikichi na wameongeza maeneo ya mengine makubwa ya hekta kwa ajili ya kuzalisha zao la alizeti na mashamba mengine waliopanga kuzalisha mazao mengine kwa kuona shida iliyojitokeza wakaona wazalishe mazao ya alizeti.

“Lengo kubwa ni kwenda sambamba na msisitizo wa seriali kuhakikisha mafuta yanapatikana nchini kwa kupatikana mbegu bora za alizeti na michikichi lakini nipende kuwakaribisha wananchi wajipatie mbegu bora za mazao kuinua nchi kiuchumi wao”Alisema

Alisema michikichi hiyo inatokana na Wakala huo kukuza miche kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) wanapata miche kutoka kwao wanaikuza na kuitoa kwa wadau mbalimbali kama walivyofanya kwa Dawasa.

Awali akizungumza wakati akipokea mbegu hizo za Michikichi, Mkuu wa Kitengo cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi Modester Mushi alisema pamoja na wao kutoa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira wanatumia maji kutoka kwenye vyanzo vya mito na hapo lengo lao linaanzia kwenye mto Ruvu ambao unawapatia maji zaidi ya asilimia 92 huduma inayotolewa Dar Es Salaam na Pwani.

Alisema kwamba wameamua kuchukua miche hiyo ya michikichi pamoja na uelekeo wa Serikali katika kuona kwamba wanataka kuzalisha mafuta nchini wao wameona ni zao ambalo litasaidia kutunza chanzo.

Aidha alisema kingo za Mito kwa hivi sasa zinaathirika kwa shughuli za binadamu ikiwemo kilimo, ufugaji hivyo shughuli hizo wananchi wanafanya ili waweze kupata mahitaji yao mbalimbali.

“Hivyo ni tuna imani kwamba upandaji zao la michikichi mwananchi badala ya kupanda mazao ya muda mfupi kupitia michikichi ataweza kuvuna mara nne kwa mwaka na atakuwa mmojawapo anachangia hatua na jitihada za serikali katika kutengeneza mafuta na kipato chake kitabadilika na kitakuwa zaidi ya hivi sasa”Alisema

Alisema miche hiyo itakapokuwa pembezoni ya mto itasaidia kupunguza shughuli za mara kwa mara zinazohusisha kugusa ardhi kulima na itapunguza kiasi kikubwa tope au mchanga ambao unatokana na shughuli hizo unaopelekea mamlaka kuwa na gharama za juu kwenye uzalishaji wa maji.

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Kanali Maulid Surumbu alisema mara kwa mara Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amekuwa akielekea Kigoma kuhamasisha zao la michikichi ili liweze kuzalishwa kwa wingi ili mwisho wa siku waweze kuondokana na tatizo la mafuta nchini.

Mkuu huyo wa wilaya aliwahamasisha wananchi wa wilaya ya Mkinga zao hilo la mchikichi hata wilaya hiyo linastawi vizuri hivyo watumie fursa ya uwepo wa shamba la mwele ambalo limepewa jukumu lakuzalisha zao la michikichi kutoa mbegu kwa wananchi.

Hata hivyo alisema wilaya hiyo wana mashamba mengi yanayomilikiwa na Taasisi, Halmashauri na watu binafsi ambapo mashamba hayo yakitumika vizuri kuzalisha zao la mchikichi nao watakuwa miongoni mwa dau watakaochangia kupunguza gharama zinazoingiwa na serikali kuagiza mafuta nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.