Na Ali Muhammed Shaaban.OMPR.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaongeza mashirikiano yaliyopo na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ili kuleta manufaa kwa pande zote mbili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameeleza hayo Ofisini kwake Vuga alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi mpya wa China Nchini Tanzania Bi Chen Mingjian alipofika Ofisini kwake leo kwa mazungumzo na kujitambulisha ofisini hapo.
Mhe hemed amesema mashirikiano kati ya Nchi hizo mbili ni ya muda mrefu tokea mwaka 1964 ambapo China imekuwa ikitoa misaada katika nyanja mbali mbali kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibari kiwemo Afya, na mambo mengine.
Aidha Mhe. Hemed ameeleza kuwa katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuweka utaratibu Mzuri wa kubadilishana uzoefu kwa wataalamu wa Sekta mbali mbali Nchini kwa ndugu zao wa China kutokana na ubobezi waliokuwa nao .
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemshukuru Balozi huyo kwa mashirikiano ya karibu na Zanzibar hasa kwa msaada wa Chanjo ya Uviko 19 aina ya Sinovac walioitoa ambapo ameeleza kuwa wazanzibaari na watanzania kwa ujumla wamenufaika na chanjo hio
Katika hatua nyengine Mhe. Hemed ameialika jamuhuri ya watu wa china kuendeleza uwekezaji nchini kupitia miradi mbali mbali kwa maendeleo ya nchi zote mbili
Nae Balozi wa Chini Tanzania Bi CHEN MINGJIAN amemuhakikisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuendeleza mashirikiano yaliyopo baina ya Nchi hizo mbili kama ilivyoasisiwa tokea mwaka 1964 na kueleza kuwa yeye ana wajibu wa kuendeleza mashirikiano hayo na kuangalia njia mbali mbali za kunufaisha mataifa hayo.
Aidha Balozi MINGJIAN amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mashirikiano anayoendelea kumpatia Balozi Mdogo wa China aliyopo Zanzibar hali hiyo inaonesha namna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inavyokuza Diplomasia kwa Mataifa mbali mbali.
No comments:
Post a Comment