Habari za Punde

TANZIA: BALOZI EMMANUEL OLE NAIKO AFARIKI DUNIA


 24/07/1951 - 30/03/22 Tanzia;

Familia ya Emmanuel Ole Naiko inasikitika kutangaza kifo cha BABA YAO, BALOZI EMMANUEL OLE NAIKO kilichotokea leo 30/03/22, nyumbani kwake Bahari Beach, Dar es Salaam. Habari ziwafikie wana familia waliopo Dar es Salaam, Monduli-Arusha na kwengine kote. 

Balozi Ole-Naiko amewahi kushika nyadhifa mbali mbali kwenye serikali ikiwemo Mkurugenzi mkuu wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Wakati wa mauti unamfika alikuwa ni balozi wa Heshima wa Botswana.

Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwake Utulivu Road, Bahari Beach, Dar es salaam

Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

2 Timotheo 4; 7

Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.