Habari za Punde

Wawakilishi wakabidhiwa kadi za Yanga.

 Makamo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mhe Hemed Suleiman Abdullah akionyesha kadi yake ya elektroniki baada ya kukabidhiwa na engineer Hersi huko Baraza Wawakilishi
 Makamo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mhe Hemed Suleiman abdullah akimkabidhi kadi ya uanachama ya kielektroniki Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mhe Zubeir Ali Maulid.


Klabu ya  Yanga imezindua na  Kukabidhi kadi mpya za uanachama zenye mfumo wa  kielektronik kwa uongozi na wapenzi wa   klabu hiyo katika tawi la Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 

Hafla hiyo ya upokeaji wa kadi hizo imefanyika katika ukumbi wa ofisi za baraza la Wawakilishi  chukwani Zanzibar na kuhudhuriwa na wajumbe mbali mbali ambao ni mashabiki wa yanga  akiwemo  Makamo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mhe Hemed Suleiman Abdullah na Spika wa Baraza la Wawakilishi mhe Zubeir Ali Maulid.

 

Akipokea kadi hizo  mhe Hemed  kutoka kwa mdhamini wa timu hiyo Injiania Hersi Said  amesitiza haja ya kuendeleza kudumisha Amani na utulivu katika viwanja vya michezo.

 

Amesema ni wajibu kwa viongozi wa michezo kuendelea kuwahamasisha mashabiki wao kufahamu kwamba michezo sio uadui wala chuki bali michezo itumike katika kuwaunganisha wananchi katika kuleta maendeleo ya michezo ndani na nje ya Tanzania.

 

Spika wa baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid ameupongeza uongozi wa timu ya Yanga kwa kuandaa kadi hizo ambazo zitaweza kutumika hata katika kufanyia malipo katika shughuli za kijamii hatua ambayo itaifanya timu hiyo kuweza kuongeza mashabiki na wanachama wapya.

 

Nae msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema hatua ya Klabu  ya Yanga kutoa kadi mpya za kieloktroniki ni kuonesha namna gani klabu hiyo inawajali wanachama wake na itaendelea kuimarisha uhusiano baina ya klabu na wananchama.

 

Jumla ya wanachama  38 wa tawi hilo wamesajiliwa na kukabidhiwa  kadi mpya za uanachama zenye mfumo wa kielektronik.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.